Home Uncategorized WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM KIBAHA MJI WATEMBELEA UJENZI WA BARABARA...

WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM KIBAHA MJI WATEMBELEA UJENZI WA BARABARA YA NJIA NANE

0

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mji Silvestry Koka akifafanua jambo kwa wajumbe 94 hawapo pichani  wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mji  katika eneo la kibamba CCM  wakati wa ziara ya kugagua mradi wa kimkakati wa ujenzi wa upanuzi wa barabara ya njia nane ya  morogoro kutokea kimara hadi Kibaha,yenye urefu wa kilometa 19.2 (PICHA NA VICTOR MASANGU)

Mwakilishi wa Meneja kutoka Wakala wa (TANRODS)  Mkoa wa Dar es Salaam  Mhandisi Issa Mbura wa kulia akiwa akimpa maelezo ya mradi wa ujenzi  wa upanua wa barabara ya njia nane  eneo la Kibamba Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mji Silvestry Koka kushoto mara baada ya wajumbe hao walipofika kuijinea shughuli zinazoendelea.(PICHA NA VICTOR MASANGU).

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mji Silvestry Koka kushoto akifafanua jambo kwa Mwakilishi wa Tanrods Mkoa wa Dar es Salaam Issa Mbura wakati wa ziara hiyo ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mji jinsi ya mwenendo mzima wa jinsi ya ujenzi unavyoendelea(PICHA NA VICTOR MASANGU).

Wajumbe wapatao 94 wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara yao ya kujionea mradi mkubwa wa kimkakati wa ujenzi wa upanuzi barabara ya njia nane ambayo inatokea kimara hadi Kibaha ambayo inajengwa na serikali kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari.(PICHA NA VICTOR MASANGU).

**********************************

VICTOR MASANGU,KIBAHA

MRADI mkubwa wa kimkakati  upanuzi wa njia nane wa barabara ya morogoro kutokea kimara hadi Kibaha yenye urefu wa kilometa 19.2 licha ya  kufikia  kiwango cha asilimia 59.1 hadi sasa  ya ujenzi wake lakini imeelezwa   bado ulikuwa unakabiliwa na changamoto ya kukwama katika baadhi ya maeneo kutokana na kuwepo kwa mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha  hivi karibuni hivyo kupelekea miundombinu mingine kuharibika.  

Hayo yalibainishwa na mwakilishi kutoka Wakala wa (TANRODS)  Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Issa Mbura wakati wa ziara  ya wajumbe  wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM)   Kibaha mji ambao wametembelea mradi wa huo ambao umefikia maeneo ya kibamba  kwa  lengo na kukagua miradi mbali mbali ya kimikakati ya  serikali ikiwa ni moja ya kujionea utekelezaji wa ilani ya chama jinsi inavyokwenda kama maagizo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli yalivyotolewa.

Kwa upande wake Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka alimpongeza  Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kwa ujenzi wa upanuzi huo wa barabara ambao utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kibaha pamoja na Taifa kwa ujumla kwani utasaidia  kuleta chachu  ya kimaendeleo na kuondokana na kero kubwa ya  msongamano wa magari  ambao umekuwa unakwamisha shughuli mbali mbali za ujenzi wa Taifa  kutokana na kupoteza muda mwingi njiani.

 

Aidha Koka aliiomba serikali ya awamu ya tano kuendelea kuiboresha miundombinu ya barabara ikiwemo kufanya upanuzi amabao utasaidia kupunguza msongamano wa magari makubwa na madogo amabayo yamekuwa ni kero kubwa hivyo kukamilika kwa mradi huo utaleta unafuu hata kwa wananchi ambao walikuwa wanasafiri kwa usafiri binafisi.

“Ofisi ya Mbunge kwa kushirikioa ana wajumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) katika KIbaha mji tumeona ni vema tufanye ziara maalumu kwa ajili ya kutembelea miradi mbali mbali ya mikakati ambayo ipo katika utekelezaji wa ilani ya chama, lengo ikiwa ni kuona mambo jinsi yanavyokenda, lakini kikubwa namshukuru sana Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha ambazo kwa sasa tunajionea matunda yake katika nyaja tofauti,”alisema Koka.

 Aidha mwakilishi huyo wa Tanrods akifafanua zaidi amesema kwamba mradi huo utakwenda wa awamu mbali mbali ambapo baada ya kukamilika mpaka Kibaha utaendelea katika mikoa mingine ya Morogoro hadi makao makuu ya nchi Dodoma lengo ikiwa ni kuzipanua barabara hizo ambazo zitasaidia kurahisiha magari kufanya safari zake kwa urahisi.

“Kwa sasa mradi huu tunaendelea nao vizuri lakini kikubwa hapa tunaendelea na ujenzi na kwa faida ya wananchi wote mradi huu kwa sasa utekelezaji wake  upo katika awamu ya kwanza, na vile vile utaendelea katika awamu nyingine hadi Mkoani Dododoma kulingana na bajeti ya fedha ambayo itakuwa ikipatikana na ujenzi huu ukikamilika utakuwa ni msaada wa kupunguza sana msongamano,”alisema.

ZIARA hiyo  ya wajumbe 94  wa halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha Mji kutoka kata zote  14  imetembelea na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ile ya kimikakati saba  ambayo inatekelezwa na serikali ya awamu ya tano ikiwemo katika  sekta, afya, maji , elimu,soko,  pamoja na miundombinu ya barabara,kwa lengo la kubaini changamoto zilizopo ili kuzitafutia ufumbuzi.