Home Mchanganyiko WAZIRI HASUNGA ATOA SIKU 23 SKIMU YA UMWAGILIAJI NANGANGA WILAYANI RUANGWA KUWA...

WAZIRI HASUNGA ATOA SIKU 23 SKIMU YA UMWAGILIAJI NANGANGA WILAYANI RUANGWA KUWA IMEKAMILIKA

0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua risiti za mauzo ya korosho wakayi alipotembelea ghala la kuhifadhia korosho la BUKO akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Narunyu katika Halmashauri ya Mtama yenye eneo la hekta 1200 zinazofaa kwa umwagiliaji wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Narunyu katika Halmashauri ya Mtama yenye eneo la hekta 1200 zinazofaa kwa umwagiliaji wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Nanganga wilayani Ruangwa wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ta Kilimo)
 Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Skimu ya Umwagiliaji ya Nanganga wilayani Ruangwa wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akipumzika kwenye magunia ya korosho yakliyohifadhiwa katika ghala la Mtama lilipo katika Halmashauri ya Mtama wilaya ya Lindi wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Lindi leo tarehe 12 Disemba 2019. 
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo- Lindi
Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa siku 23 pekee kwa wakandarasi wanaojenga
Skimu ya Umwagiliaji ya Nanganga wilayani Ruangwa kuwa wamekamilisha ujenzi wa
mradi huo.
Waziri
Hasunga ametoa agizo hilo leo tarehe 12 Disemba 2019 la kukamilika kwa mradi
huo wakati alipotembelea na kukagua skimu hiyo yenye hekta zipatazo 300 akiwa
katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Lindi.
Amesema
kuwa mradi huo unaohusisha ujenzi wa banio katika mto Lukuredi, mfereji mkuu
wenye urefu upatao mita 525, mfereji wa kati wenye urefu upatao mita 2675,
mifereji midogo vigawa maji pamoja na vivuko vya miguu ulipaswa kukamilika
Julai 2, 2019 lakini mpaka sasa umeshindwa kukamilika kwa wakati jambo ambalo
limewakosesha wakulima fursa ya kilimo cha umwagiliaji.
“Mkandarasi
aliomba aongezwe muda wa miezi mitano baadaye ameongezwa tena mwezi mmoja
lakini mpaka sasa ameshindwa kukamilisha nadhani ameamua kutuchezea akili
hatutakubaliana na hilo hata kidogo” Alikaririwa Mhe Hasunga
Akizungumza
na wananchi wa Kijiji na kata ya Namanga Mhe Hasunga amesema kuwa miradi mingi
ya umwagiliaji nchini haikamiliki kwa wakati kutokana na wakandarasi
kutotekeleza majukumu yao ipasavyo.
“Haiewezekani
Waziri Mkuu anayechapa kazi, anahangaika nchi nzima kila kona halafu kwake ndio
mradi uwe haujakamilika hivi tutakuwa na akili timamu kweli hilo halikubaliki”
Alisema
Amemtaka
mkandarasi kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika ndani ya muda uliokubaliwa
vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Waziri
Hasunga amesema kuwa serikali inajipanga na mkakati kabambe wa kuhakikisha kuwa
hakutaanzishwa miradi mipya ya umwagiliaji mpaka pale miradi iliyoanzishwa
itakapokuwa imekalmilika.
 
Kuna
miradi mingi imeanzishwa lakini haijakamilika ilihali kiasi kikubwa cha fedha
kinakuwa kimetumika.
Mradi wa
umwagiliaji Nanganga ni kati ya miradi 16 ya SSIDP III (Small Scale Irrigation
Development Project) awamu ya tatu iliyojengwa na serikali ya Tanzania chini ya
wizara ya Kilimo na kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC).
Katika
ziara hiyo ya kikazi Waziri Hasunga ametembelea na kukagua skimu ya umwagiliaji
Narunyu katika Halmashauri ya Mtama yenye eneo la hekta 1200 zinazofaa kwa
umwagiliaji.
Vilevile Waziri
Hasunga ametembelea na kukagua ghala la kuhifadhia korosho la BUKO kadhalika
ghala la kuhifadhia korosho la Mtama ambapo amepongeza utunzaji wa korosho za
wakulima katika maghala hayo.