Home Mchanganyiko KITABU CHA MTOTO WA MIAKA 8 “BIBLIA YANGU” CHA ZINDULIWA KWENYE FURSA...

KITABU CHA MTOTO WA MIAKA 8 “BIBLIA YANGU” CHA ZINDULIWA KWENYE FURSA YA DAR

0

Mtoto
Samwel Michael Gimeno (miaka 8) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake

 MAMA Mzazi wa Samweli Suzana Senso akizungumza wakati wa uzinduzi huo

 Mkurungezi wa Fursa Bi Suma Mwaitenda kulia akimkabidhi kitabu hicho Samweli mara baada ya kufanya uzinduzi

 MAMA
Mzazi wa Samweli Suzana Senso kushoto akimpatia nakala ya kitabu
kilichoandikiwa na Mwanae Mtangazaji wa Kipindi cha Njia Panda cha
Clouds FM Radio Dkt Isaac Maro wakati wa uzinduzi huo

Mtoto
Samwel Michael Gimeno (miaka 8) akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake na mdogo wake Alan Michael Gimeno

Mtoto
Samwel Michael Gimeno (miaka 8)
katikati akiwa kwenye picha mara baada ya uzinduzi wa kitabu chake

Jumamosi tarehe 7/12/2019  ilikuwa siku ya pekee wa mtoto
Samwel Michael Gimeno (miaka 8) ambae alibahatika kuzindua kitabu chake
cha kwanza ndani ya fursa ya Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Julius
Nyerere International Conference Center


Kitabu cha BIBLIA YANGU kilizinduliwa na Mkurungezi wa Fursa Bi Suma Mwaitenda


Samwel amekuwa mtoto wa pekee kwenye familia ambae Mungu
Ameweka kipaji cha kuandika na kuchora na Sisi kama wazazi wake tumeamua
kumsaidia ili kuiishi ndoto yake maneno hayo yamesema na mama mzazi wa
Bi Suzana Senso


Kitabu cha kwanza cha Samwel kitakwenda Kuwa kinatolewa kwa
watoto Yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ikiwa sehemu ya
samwel kurudisha kwa watoto wezake wanaoishi kwenye mazingira magumu
ambao ni mara chache sana kupata kitabu kinzuri na chenye hadithi za
kwenye Biblia kutokana na mazingira wanayoishi maneno hayo yamesemwa na
baba wa Samwel Bw Michael Samwel Gimeno


KAMPENI KALAMU YANGU
Ni maneno yatakayo kwenda kutumika kwenye  kampeni samwel ambayo itakuwa
nikutembelee vituo vya  watoto yatima na watoto wanaoishi kwenye
mazingira magumu na  kuwagawia vitabu ili nao waweze kusoma sio tu
kusoma kitabu tu ila pia kusoma kitabu kilichoandikwa na mtoto mwezao


Kampuni hii inaanza mwezi huu wa 12 hadi siku ya wapendanao
tarehe 14/2/2020 ambapo samwel atakwenda kula na watoto wanaoishi
kwenye kituo cha watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu
ambacho tutakitaja siku zijazo na pia kuwagaia vitabu ya BIBLIA YANGU


Gharama ya kitabu itakuwa shilingi elfu 20,000 kuanzia 15/2/2020 baada ya kampuni ya KARAMU YANGU ukisha tarehe 14/2/2020


Mama Samwel alisema Kwa sasa tunatamani kupata watu wa ku
support kutoa nakala ya  vitabu ambavyo tunatajia kuvigawa kwenye vituo
vya watoto yatima Kwani hii kampeni haina mfadhili wa kufanya Ila ni
wazazi tu  ndio tunaifanya na tunatamani kuwafikia watoto wengi sana
Kwa yeyote atakae wiwa kuungana nasi kwenye Hii kampuni anaweza ku wasiliana Kupitia namba 0736 372138


Tukiwa kama wazazi wa Samwel tunapenda kuwashukuru Joel Kiiya ambae ni
mentor wa Samwel, Bi Ezabel Simuyu ambae ndie ame design kitabu,
photography wake Muki, Emanuel, Mkurungezi wa Fursa na wale waliotumia
muda wao kufanikisha kitabu cha “BIBLIA YANGU” hadi kutoka.


MUNGU AWABARIKI