Home Biashara RC.MWANRI AMEMPONGEZA MSANII ALIKIBA KWA MCHANGO WA VIFAA TIBA KATIKA MKOA WA...

RC.MWANRI AMEMPONGEZA MSANII ALIKIBA KWA MCHANGO WA VIFAA TIBA KATIKA MKOA WA TABORA

0

**********************

Msanii wa kizazi kipya hapa nchini AliKiba amepongezwa na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kwa mchango wake wa vifaa tiba vya zaidi ya shilingi Milioni 6 kwa wananchi wa mkoa huo.

AliKiba alikabidhi vifaa hivyo kwa Aggrey Mwanri ikiwa ni sehemu ya kurejesha shukrani zake kwa wananchi wa Tabora katika tamasha lake ‘AliKiba Uforgetable Tour’ litakalofanyika Novemba.