Home Mchanganyiko Viongozi wa Dini kushiriki Mapambano Dhidi ya Kifua Kikuu

Viongozi wa Dini kushiriki Mapambano Dhidi ya Kifua Kikuu

0

 Viongozi wa
dini mbalimbali nchini Tanzania wanatarajiwa kukutana jijini Mwanza ili kwa
pamoja kusaini maazimio ya kushiriki kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa Kifua
Kikuu (TB) kupitia nyumba zao za ibada.
 
Mwenyekiti
wa kambi rasmi ya wabunge wanaopambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu, Oscar Mkasa (kuli) ameyasema hayo Novemba 27, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari
mkoani Mwanza kuhusiana na shughuli hiyo.
 
Mkasa ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya
Ukimwi, Kifua Kikuu na Madawa ya Kulenya amesema shughuli hiyo inatarajiwa
kufanyika Ijumaa Novemba 29, 2019 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mwanza.
 
Naye Mkuu wa
Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) amebariki shughuli hiyo akisema itasaidia kutoa
elimu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu ambao takribani asilimia
sita ya wagonjwa wote nchini wanatoka mkoani humo.
Na George Bingai-GB Pazzo, Mwanza