***************************************
Getrude Alex (40), Afisa wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora amefariki dunia usiku wa Novemba 23, 2019 katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Marehemu alikutwa na umauti baada ya kupata ajali ya kugongwa
na pikipiki Novemba 21, 2019 katika eneo la ubungo jijini Dar es
Salaam na kukimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa
matibabu.
Marehemu aliajiriwa na tume Oktoba 18, 2010 kama Afisa
Uchunguzi mwenye taaluma ya habari, na mpaka kifo kinamkuta
alikuwa amehudumu katika taasisi hiyo kwa takribani miaka tisa
(9).
Historia yake ya maisha inaonesha kuwa marehemu alikuwa mama
wa watoto watatu wa kiume ambao ni Tupendane, Mbarikiwa na
Baraka.
Kitaaluma marehemu alikuwa ni msomi wa Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari (SJMC) mwenye
Shahada ya Habari (2007).
Marehemu alizaliwa jijini Mwanza Julai 7, 1979. Alianza masomo
shule ya msingi Kirumba (1989-1995), baadae alichaguliwa na
kujiunga Mwanza Sekondari ambapo alimaliza elimu ya kidato cha
nne (1996-1999).Kidato cha sita alimaliza katika shule ya
Sekondari Tagwa (2000-2003).
Marehemu ataendelea kukumbukwa kwa wema wake, ucheshi,
ushirikiano wake kwa watumishi hasa katika mambo ya kijamii na
ukarimu.
Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.