UCHAGUZI UJAO NI FURSA KWA WANAWAKE KUSHIRIKI UCHAGUZI HUO

  0

  ***********************************

  Na Masanja Mabula –Pemba……22/11/2019

  NCHI ya  Tanzania ni moja ya nchi zinazofuata misingi ya demokrasia kwa kufanya uchaguzi kila baada ya kipindi cha miaka mitano.

  Utaratibu huo uliowekwa ni ushahidi tosha kwamba nchi ya Tanzania ni nchi inayozingatia misingi ya utawala bora , ambapo viongozi wanabadilishana kila baada ya kipindi cha miaka kumi kwa ngazi ya Urais.

   Kwa maantiki hiyo  uchaguzi Mkuu wa Tanzania umekaribia ambapo kwa  sasa tumesalia na miezi  kaddaa  ili tuingie kwenye  mchakato wa uchaguzi   utakaofanyika mwaka 2020.

  Wakati uchaguzi  Mkuu ukiwa unakaribia ni budi wanawake wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi wakaanza kujitafakari na kujitathimini  mapema  kabla ya uchaguzi huo.

  Ni nafasi pekee kwa wanawake kujitathimini  na kujipima uwezo wao wa kuongoza ili kuweza kushindana na  wanaume  kuwania nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya wadi na majimbo.

  Lengo la 50  kwa 50, haliwezi kufikiwa iwapo wanawake hawataondoa fikra ya kusubiri nafasi za uteuzi au nafasi maalum.

  Nimekuwa nikifuatilia sana chaguzi kupitia nafasi za wanawake ,hapa huwa kuna upinzani mkubwa  , kuliko ule mchakato  wa majimboni.

  Nafasi hizi ambazo ni maalumu kwa wanawake, utakuwa wanawake wenye na uwezo  wa kuongoza na kutoa ushindani  kwa wanaume wanashiriki kuwania nafasi za uteuzi.

  Maswali mengi huwa najiuliza kwa nini wanawake hawa wenye uwezo wa kuongoza  majimbo wanasubiri nafasi hizi, jibu ni kwamba hata kama watagombea nafasi za majimbo wanawake wenzao ndio ambao wanawavunja moyo kwa kutowaunga mkono.

  Hakuna ubishi kwamba wakati wa kampeni , wapo baadhi ya wanawake wanaosimama na kuanza kuwafanyia kampeni wanaume na wakashinda , je  wanawake hawa kwa nini wasiwaunge mkono wanawake wenzao wanaogombea , jibu ni lile lile la kwamba hawapendani.

   Serikali za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kweli zimejitahidi  kuteuwa wanawake kadhaa kushika nyadhifa mbali mbali za uongozi, lakini lile lengo la 50 kwa 50 bado haalijafikiwa.

  Pamoja na wanaharakaati wanaotetea haki za wanawake kudai nusu kwa nusu, changamoto niliyoibaini ni kwamba wanawake  kama hawatabadilika kwa kundoa dhana  ya kudharauriana lile lengo  la 50 kwa 50 haliwezi kufikiwa.

  Changamoto hiyo ya wanawake kutopendana , inatoa mwanya kwa wanaume kuendelea kupeta na kujimilikisha majimbo kana kwamba  wanawake hawawezi kuongoza.

  Wanawake wanapaswa kubadilika na kuhakikisha wanasimama kidete kuwapigia kura wanawake  wenzao wanaojitokeza kugombea nafasi za uongozi tukiamini kwamba wanawake bila ya kuwezeshwa wanaweza.

  Wapo wanawake wenye nia na uwezo wa kuongoza , hebu tuwapime na tuwape nafasi hiyo kwani wanauwezo mkubwa wa kutetea haki za jamii kuwa wao ndiyo walezi wa familia.

  Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Mkoa wa Kaskazini Pemba wenye  majimbo tisa ya Uchaguzi ni wanawake watatu tu ndio waliokuwa wagombea wa nafasi ya uwakilishi kupitia mmoja ya chama cha Siasa.

  Mfumo dume huu unaanzia kwenye vyama vya siasa wakati wa kuchagua wagombea wao wataowawakilisha kwenye uchaguzi Mkuu ambapo wanawake hunyimwa fursa aidha kutokana na maumbile yao ama imani pamoja na mila potofu juu ya mwanamke.

  Tunapoelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020,  kila mmoja anapaswa kuchukua hatua kusimamia maendeleo ya mwanamke  pamoja kumshamasisha mwanamke kugombea nafasi za uongozi.

  Ule msemo wa kwamba nguo ya Ijumaa hufuliwa Alhamisi unafaa aunze kufanya kazi ili ikifika siku husika iwe tayari kuvaliwa.

  Ni imani yangu kwamba msemo huu iwapo utapewa fursa na kufanyiwa kazi, maendeleo na malengo ya wanawake yatafikiwa na hivyo kufikia ile 50 kwa 50.

  Ni lazima ifahamike kwamba sina maana ya kuwataka wanawake kuanza kufanya kampeni  lahasha , ninachojaribu kukizungumzia hapa ni ule mpango wa wanawake kujitathimini ikiwa wanania ya kugombea nafasi majimboni.

  kutokana na uchambuzi wangu , naomba nisileke vibaya kwani nia na lengo langu ni kuonyesha jinsi mwanamke analivyo na nafasi wa kuongoza sawa na mwaname.

  Niwaombe sana wanawake kubadilika na kuondoa dhana ya kutopendana bali wadumishe ushirikino kwa kuungana mikono wakati  wanapotaka kugombea nafasi kwa kushindana na wanaume .

  Hivyo basi wewe mwanamke popote ulipo chukua hatua na kumuunga mkono mwanamke mwenzako ambaye ataonyesha nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha uongozi kuanzia ngazi ya wadi.