Home Biashara TBS YAKAMATA VIPODOZI VYENYE VIAMBATA SUMU SINGIDA

TBS YAKAMATA VIPODOZI VYENYE VIAMBATA SUMU SINGIDA

0

***********************************

Shirika la Viwango Tanzania limekamata vipodozi vyenye viambata sumu katika ukaguzi uliofanyika Mkoani Singida.Ukaguzi huo umefanyika Mkoani hapo kuanzia Novemba 11, mwaka huu na Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na linatarajiwa kuhitimishwa Novemba 25, mwaka huu.

Ukaguzi huo wa kushtukiza uliofanyika kwenye maduka ya kuuza vipodozi na kufanikiwa kukamata vipodozi vyenye viambata sumu, ambavyo vimepigwa marufuku kutokana na kuwa na madhara kwa binadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari Manyoni leo Mkaguzi wa Shirika hilo, Domisiano Rutahala alisema kwamba zoezi hilo limefanyika Singida maeneo ya Singida Manispaa, Kiomboi , Shelui,Mkalama,itigi na Manyoni

“Tumefanikiwa kukamata vipodozi vyenye viambata sumu ambavyo vimepigwa marufuku kutokana na kuwa na madhara kwa watumiaji.Vipodozi hivyo vinaondolewa kwenye soko kutokana na kuwa na madhara mbalimbali kwa watumiaji. Alisema Rutahala

Aliongezea pia Baadhi ya madhara ya vipodozi hivyo ni kusababisha saratani ya ngozi, kupunguza kinga ya ngozi na kuathiri mfumo wa homoni za mwili.

Rutahala, aliwashauri watumiaji kuacha kutumia vipodozi vilivyopigwa marufuku na kutoa wito kwa wafanyabiashara kuacha kuviuza.

Wakati huo huo, shirika la Viwango limewataka wenye maduka ya chakula na vipodozi kujisajili kupitia mfumo unaopatikana kwenye tovuti ya shirika hilo, ili waweze kupatiwa vibali vinavyotakiwa kwa ajili ya kufanya biashara hizo.