Home Mchanganyiko MUWSA WAMUOMBA WAZIRI WA MAJI ,PROF MAKAME MBARAWA KUSAIDIA KUKUSANYA MADENI YA...

MUWSA WAMUOMBA WAZIRI WA MAJI ,PROF MAKAME MBARAWA KUSAIDIA KUKUSANYA MADENI YA MAJI KWA TAASISI ZA SERIKALI

0
Waziri wa Maji ,Prof Makame Mbarawa akizingumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) .
Baadhi ya Wafanyakazi 
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya MUWSA waliomaliza muda wao na wale wapya wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Prof Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa kutamburisha wajumbe wapya wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) 
Baadhi ya Wafanyakaziw  wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya MUWSA iliyomaliza muda wake na wajumbe wapya wa Bodi hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakifuatilia kwa karibu hotuba zilizokuwa zikitolewa katika hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya . 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,Moshi
aliyemaliza muda wake ,Prof Faustine Bee akizungumza wakati akitoa taarifa ya Bodi iliyomaliza muda wake na kukabidhi kwa Bodi mpya .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,Patrick Boisafi akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA). 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,Moshi
aliyemaliza muda wake ,Prof Faustine Bee (kulia ) akikabidhi nyaraka za
Bodi hiyo kwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya MUWSA ,Prof  Jafari Kidegesho
mara baada ya Waziri kuizundua rasmi mjini Moshi
Wajumbe wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka mjini Moshi (MUWSA) . 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Prof Makame Mbarawa akikabidhi vitendea
kazi kwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira ,(MUWSA) ,Prof Jafary Kidegesho wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo ulifanyika zilipo ofisi za MUWSA
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Prof Makame Mbarawa akikabidhi vitendea
kazi kwa katibu wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira ,(MUWSA) ,Mhandisi Aron Joseph ambaye pia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka hiyo .Hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo umefanyika
zilipo ofisi za MUWSA
Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi ,Joyce Msiru ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ,akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Maji,Prof Makame Mbarawa mara baada ya Bodi hiyo kumaliza muda wake. 
Waziri
wa Maji ,Prof Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na
Wajumbe wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi
,(MUWSA) mara baada ya kuizindua .  
 Waziri
wa Maji ,Prof Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na
Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,Moshi waliomaliza muda wao ,tukio hili limefanyika  wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaka hiyo.    
Waziri wa Maji ,Prof Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi ,(MUWSA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaka hiyo.  
 

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}

Na Dixon Busagaga ,Moshi
WAFANYAKAZI  wa Malmala ya Majisafi na Usafi wa MAzingira
,Moshi,(MUWSA) wamemuomba Waziri wa Maji ,Prof Makame Mbarawa kusaidia mchakato
wa kufuatilia fedha za malimbikizo ya madeni ya maji kwa taasisi za serikali
ambazo ni zaidi ya Sh Bil 2.3.
Mamlaka ya Majisafi an Usafi wa Mazingira
mjini Moshi (MUWSA) ni miongoni mwa mamlaka zinazotajwa kufanya vizuri katika
utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi inaowahudumia ambapo kwa sasa imefikia wastani
wa asilimia 91% kwa eneo inayohudumia.
Licha ya mafanikio hayo
yanayoitamburisha MUWSA kuwa miongoni mwa Mamlaka Bora nchini ,changamoto iko
kwenye Madeni yatokanayo na Ankara za maji kutoka kwa taasisi za serikali .
Akizungumza wakati wa kuzindua bodi
hiyo Waziri wa Maji, Prof.Mbarawa amesema Wizara kwa sasa imelekeza nguvu zake
kwenye kusimamia makusanyo katika Mamlaka za Maji nchini ili kuweza kufikisha
huduma ya maji katika maeneo mengi zaidi.
Katika hafla fupi ya uzinduzi wa
Bodi Mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ,Moshi (MUWSA) Waziri
Mbarawa alisema ‘Wakati wangu wote natumia nguvu nyingi kusimamia makusanyo
kwenye mamlaka za maji, ziko ambazo zikitaka hata kufunga nati kwenye miradi zinakuja
wizarani kuomba fedha”alisema Prof Mbarawa.
Zaidi Mbarawa aliongeza: “Mamlaka
hizi kama tutazisimamia vizuri zina uwezo mkubwa sana, lakini bado tuko kwenye
usingizi. Nataka kila bodi mpaka watendaji wabadilike na kuiga mfano wa Mamlaka
ya Maji ya Moshi Mjini”alisema .
“Mimi baada ya kuingia katika Wizara
hii niliamua kuzifuatilia mamlaka kama saba ambayo ni Dar es Salaam, Moshi,
Arusha, Morogoro, Mbeya na mamlaka za maji ndogo ndogo za Kilwa na Makonde.”
Alisema kasi ya ukusanyaji wa mapato
kwa Muwsa, inampa moyo wa kuendelea kukaa katika Wizara hiyo hasa kutokana na
takwimu kuonyesha kuna jitihada za kuongeza makusanyo yake kila mwezi.
“Mimi ukiniuliza, nasema Muwsa ina
uwezo wa kukusanya Sh. bilioni 1.2 kwa mwezi na hilo halina ubishi, kwa sababu
mwezi Januari 2019 tulikuwa tumekafika Sh. milioni 814,”alieleza Mbarawa
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka
hiyo, Mhandisi Aron Joseph amesema hali ya utoaji wa huduma ya maji kwa sasa
inaridhisha, kutokana na kutoa huduma katika kata 21 zilizopo ndani ya Manispaa
ya Moshi na Wilaya ya Hai na Moshi Vijijini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof.
Kitila Mkumbo akizungumza kabla ya Waziri Mbarawa kuhutubia, alisema kulikuwa
na utitiri wa mamlaka za maji 159 nchi nzima lakini mamlaka hizo zimepungua
sasa na kufikia mamlaka 83.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Muwsa
aliyemaliza muda wake, Prof. Faustine Bee ambaye kwa sasa ni Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alimweleza Waziri Mbarawa kuwa mpaka wanaondoka
katika nafasi hiyo, deni la ankara za maji katika taasisi za umma ni Sh.
bilioni 2.16
Pia, alimweleza kuwa mkakati
mahususi waliouacha mchakato wake uendelezwe na bodi mpya ni pamoja na upanuzi
wa mabwawa ya majitaka yanayopokea majitaka kutoka maeneo mbalimbali ambao
gharama zake zinafikia Sh. bilioni 7.6