Home Mchanganyiko MHE HASUNGA AAGIZA VIONGOZI WA AYALABE DAIRY NA AYALABE SACCOS WILAYANI KARATU...

MHE HASUNGA AAGIZA VIONGOZI WA AYALABE DAIRY NA AYALABE SACCOS WILAYANI KARATU WAKAMATWE

0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi
kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu wakati akiwa kwenye
ziara ya kikazi mkoani Arusha tarehe 10 Novemba 2019. (Picha Zote Na Mathias
Canal, Wizara ya Kilimo)

Sehemu ya wanachama wa Chama cha Akiba na mikopo cha Ayalabe na na
Chama cha Ushirika wa Ayalabe Dairy wilayani Karatu wafatilia mkutano
ulioongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) sambamba na Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani
Arusha tarehe 10 Novemba 2019.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) sambamba na Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mhe Mrisho Gambo wakiwasikiliza wananchi kwa umakini mkubwa wakati wa
mkutano na wanachama wa Chama cha Akiba na mikopo cha Ayalabe na na Chama cha
Ushirika wa Ayalabe Dairy wilayani Karatu wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi
mkoani Arusha tarehe 10 Novemba 2019.
Sehemu ya wanachama wa Chama cha Akiba na mikopo cha Ayalabe na na
Chama cha Ushirika wa Ayalabe Dairy wilayani Karatu wafatilia mkutano
ulioongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) sambamba na Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani
Arusha tarehe 10 Novemba 2019.
 
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Arusha
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) ameliagiza jeshi la Polisi Mkoani Arusha kwa kushirikiana na Mkuu
wa Upelelezi, na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)
kuwakamata viongozi mbalimbali wa Chama cha Akiba na mikopo cha Ayalabe na na
Chama cha Ushirika wa Ayalabe Dairy kutokana na ubadhilifu wa fedha za
wanachama wa vyama hivyo.
Waziri Hasunga ametoa maagizo hayo
leo tarehe 10 Novemba 2019 wakati mara baada ya kusikiliza malalamiko ya
wanachama wa vyama hivyo wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika eneo la
uwanja wa vyama hivyo Wilayani Karatu ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya
kikazi ya siku mbili mkoani Arusha.
Waziri
Hasunga ameagiza viongozi hao kukamatwa haraka iwezekanavyo kwani dhamira ya
serikali ya awamu ya tano ya kuanzisha vyama vya ushrika ni kuwanufaisha
wananchi kupitia umoja huo.
Viongozi
hao ni Wajumbe wa Bodi ya AYALABE SACCOS ambao ni aliyekuwa Mwenyekiti Ndg
Christopher Kastuli, Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Ndg Yuda Moratha, Waliokuwa
makatibu Bi Maria Lohay na Anastazia Evodi pamoja na wajumbe Eustela Kastuli,
Faustini Tekko, Ludovick Marmo, Tarsila Visent na Costantine Matle.
Wengine ni waliokuwa wajumbe wa
Chama cha Ushirika wa Ayalabe Dairy ambao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa chama
hicho Yuda Moratha, aliyekuwa Makamu mwenyekiti Faustine Tekko, aliyekuwa
katibu wa chama hicho Ndg Yasinta Faustin, na wajumbe ambao ni EufrasiaAntony,
Israel Sarwat, Evarist Sulle, Florance Neston na Eustela Kastuli.
Waziri Hasunga ameagiza pia kukamatwa
viongozi wote wa makampuni yaliyochukua hela kinyume na taratibu za ushirika,
kampuni hizo ambazo ni Shimaswa na Teddy Agrovet.
Katika hatua nyingine ameagiza Ndg
Blanka Michael akamatwe kutokana na kukodisha eneo la Chama cha Ushirika wa
Ayalabe Dairy pasipo kufuata utaratibu wa kisheria.
Katika mkutano huo pia Mhe Hasunga
ameagiza kuwekwa kizuizini viongozi na wajumbe wa kamati ya usimamizi wa Chama
cha Akiba na mikopo cha Ayalabe ambao ni aliyekuwa Mwenyekiti Ndg Lazaro Titus
Lazaro  na wajumbe Joseph Bayo na Eudesi
Jonas.
Waziri Hasunga ameuagiza uongozi
uliopo wa Chama cha Ushirika cha akiba na mikopo cha Ayalabe kusitisha mara
moja kulipa deni la mkopo waliochukua wa shilingi 500,00,000 kutoka Benki ya
TIB kwa kutumia hati za majengo ya Ayalabe Dairy mpaka serikali
itakapojiridhisha kama mkopo huo ni halali.
Ameagiza watuhumiwa hao wote wafunguliwe
kesi ya uhujumu uchumi na watakaoweza kurudisha fedha za wanachama waweze
kusamehewa. Pia ameuagiza uongozi wa wilaya ya Karatu na Tume ya Maendeleo ya
Ushirika kuhakikisha kuwa wanasimamia ukarabati wa kiwanda cha Ayalabe Diary na
kufikia mwezi Januari 2020 kianze kufanya kazi.
Chama cha Ushirika wa maziwa cha
Ayalabe kilipokea kiasi cha shilingi 513,407,077 kutoka Halmashauri ya Wilaya
ya Karatu kupitia miradi ya ASDP na DADPS tangu mwaka 2009 hadi 2013 kwa ajili
ya ujenzi wa kuboresha kiwanda cha maziwa ambapo hata hivyo baada ya kufanyiwa
uchunguzi na ukaguzi kilibainika kuwa na ubadhilifu wa Tshs 147,126,000 huku
chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) chenyewe kilikuwa na akiba za
wanachama ambazo ni shilingi 11,015,000 na hisa zao zilikuwa Tshs 2,830,000,
huku kikiwa kimechukua mkopo wa Tshs 500,000,000 kutoka Benki ya TIB.