MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akihutubia wakati hafla ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar,huduma hiyo imetolewa na Madaktari Bingwa wa Kichina, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja.kushoto Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar.Mhe.Maudline Castico, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Uwezeshaji wa Wazee, Wanawake na Watoto Zanzibar.Bi. Fatma Gharib Bilal, Naibyu Waziri.Mhe.Shadya Mohammed na Mkuu wa Wilaya ya Mjini.Bi.Marine Thomas Joe.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akihutubia wakati hafla ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba za Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar,huduma hiyo imetolewa na Madaktari Bingwa wa Kichina, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja.kulia Mke wa Balozi Mdogo wa China Zanzibar.Bi.Liu Jie, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi na Makamu Mwenyekiti wa UWT.Bi. Thuwaiba Editin Kisasi.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akishuhudia huduma ya Uchunguzi wa Afya kwa Wazee wa Sebleni na Welezo ikitolewa na Daktari Bingwa kutoka Jamuhri ya Watu wa China.Dr.Yang Xiaodong wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa nyumba za Wazee Sebleni Wilaya ya Mjini Unguja, (kulia kwa Mama Mwanamwema Shein) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.Mama Asha Suleiman Iddi.(Picha na Ikulu)
WAZEE wa Nyumba ya Wazee Sebleni na Welezo Zanzibar wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar.Mama Mwanamwema Shein, akihutubia na kuzindua Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee inayotolewa na Madaktari Bingwa wa Kichina katika ukumbi wa Sebleni kwa Wazee.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akikabidhiwa baadhi ya Vifaa vya Afya kwa Ajili hya Nyumba za Wazee za Welezo na Sebleni na Mke wa Mdogo wa Jamuhri ya Watu wa China Anayefanyia Kazi zake Zanzibar.Bi. Liu Jie, wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba ya Sebleni na Welezo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa makaazi yua Wazee Sebleni Wilaya ya Mjiniu Unguja, kushoto Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar.Mhe. Maudline Castico.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akikabidhiwa baadhi ya Vifaa vya Afya kwa Ajili hya Nyumba za Wazee za Welezo na Sebleni na Mke wa Mdogo wa Jamuhri ya Watu wa China Anayefanyia Kazi zake Zanzibar.Bi. Liu Jie, wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Huduma ya Upimaji wa Afya kwa Wazee wa Nyumba ya Sebleni na Welezo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa makaazi yua Wazee Sebleni Wilaya ya Mjiniu Unguja.(Picha na Ikulu).
******************************
Zanzibar Novemba 2, 2019
MKE wa Rais wa Zanzibar, mama Mwanamwema Shein amesema kwa
kuzingatia umuhimu wa wananchi kuwa na afya bora, Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar imeweka kipaumbele katika sekta ya Afya, kwa kuimarisha
huduma mbali mbali .
Mama Mwanamwema amesema hayo katika uzinduzi wa huduma za
upimaji afya kwa wazee wanaoishi katika nyumba za wazee Sebleni na
Welezo, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Sebleni, mjini hapa.
Timu ya madaktari bingwa kutoka Jamuhuri ya watu wa China,
wakishirikiana na madaktari wazalendo wameendesha zoezi la upimaji wa
Afya kwa wazee wanaoishi katika nyumba hizo na kutoa huduma za
uchunguzi, dawa na ushauri.
Alisema ili kufanikisha dhamira hiyo, Serikali imechukuwa hatua mbali
mbali, ikiwa pamoja na kuimarisha miundombinu, kununua vifaa vya kisasa
vya uchunguzi, kuongeza bajeti ya dawa, kuongeza madaktari pamoja na
kusomesha vijana wake ndani na nje ya nchi.
Alisema hivi sasa huduma za za Afya katika hospitali na vituo vya Afya
kote nchini zimeimarika na kutolewa bure , ikiwa ni hatua ya kufanikisha
malengo ya muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu mzee Abeid
Amani Karume.
Alieleza kuwa hatua ya washirika wa maendeleo, ikiwemo Jamuhuri ya
Watu wa China, kuunga mkono juhudi hizo kwa wataalamu wake kupima
afya za wazee hapa nchini, ni jambo la kutia moyo na linalopasa
kupongezwa.
“Kuwapima afya wazee wetu ni kuendeleza jitihada za kuwaenzi na
kuwahudumia wazee wetu, hakika wazee hawa walifanya kazi ya kutulea
na kuijenga nchi yetu, hii ni kuonyesha tunawathamini, tunawajali na
tunawapenda”, alisema.
Aliwataka wazee hao kuitumia vyema fursa waliyoipata na kutoa
ushirikiano kwa wataalamu hao, ili kufikia malengo yaliokusudiwa.
Aidha, alitowa wito kwa wazazi na walezi kote nchini kusimamia vyema
malezi ya watoto wao kwa kuzingatia maadili mema, utamaduni na silka za
Wazanzibari, ili hatiame waweze kuwa raia wema.
Mama Mwanamwema alisitiza haja ya kuwahimiza watoto kuzingatia
masomo yao ya skuli na madrasa pamoja na kuwafuatilia nyendo zao ili
kuwaepusha na vitendo viovu, udhalilishaji na matumizi ya dawa za
kulevya.
Alitowa shukrani kwa timu hiyo ya madaktari kwa mara ya pili kukubali
kutoa huduma za upimaji wa afya, hatua aliyobainisha inaonyesha mapenzi
makubwa na urafiki uliopo kati ya wananchi wa China na Zanzibar.
Aidha, mama Mwanamwema alitowa ombi maalum kwa Ubalozi mdogo wa
China uliopo Zanzibar akiomba huduma hizo zifikishwa kisiwa Pemba kwa
ili wazee wanaoishi katika nyumba za wazee Limbani, nao waweze
kufaidika.
Altowa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwa kutimiza miaka tisa ya uongozi
wake na kubainisha maendeleeo makubwa ya kiuchumi na kijamii
yaliofikiwa.
Mapema, Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha
Suleiman Idd, aliwashukuru madaktri hao kwa moyo wao wa kujitolea na
kuona umuhimu wa kuwaenzi na kuwahudumia wazee wa Zanzibar.
Aidha, aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya Chama cha
Mapinduzi kwa kuwajali na kuwathamini wazee.
Nae, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, wazee, wanawake na watoto, Moudline
Castico alipongeza juhudi endelevu za Mama Mwanamwema na Mama
Asha Suleiman , ambapo kwa nyakati tofauti wamekuwa mstari wa mbele
kutoa misada mbali mbali ya kijamii kwa wazee na watoto wanaolelewa
katika nyumba za Serikali.
Alisema wazee wamekuwa wakikabiliwa na magonjwa mbali mbali,
ikiwemo sukari, shinikizo la damu, kiharusi, macho, masikio na mengineyo,
hivyo akabainisha hatua ya Ubalozi wa China kuedesha zoezi hilo kuwa ni
ya kupongezwa.
Alimpongeza Mke wa Balozi mdogo wa China Bi Liu Jie kwa juhudi kubwa
alizochukuwa kufanikisha kazi ya kuwapima afya wazee, hatua aliyoeleza
inayonesha imani na mapenzi kwa wazee hao.
Aidha, Mke wa Balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar, Liu Jie aliipongeza
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya uongozi wa Dk. Shein kwa
juhudi mbali mbali inazozichukuwa kudumisha amani na kuimarisha
uchumi.
Alisema China itaendelea kuiunga mkoni Zanzibar katika dhamira zake za
kuimarisha uchumi, sambamba na kuendeleza mashirikiano yaliopo kati ya
nchi mbili hizo.
Alisema ushirikiano kati ya China na Zanzibar ni wa kihistoria, hivyo
akaahidi kuendelezwa na kubainisha upimaji wa afya kwa wzee hao ni
hatua inayoonesha heshima na upendo.
Nao, wazee mbali mbali waliopatiwa huduma hizo, wameishukuru Serikali,
Ubalozi mdogo wa China pamoja na Mke wa Rais wa Zanzibar kw
akufanikisha zoezi hilo muhimu.
Wamesema wamefurahishwa kupata fursa hiyo, kwani imemwawezesha
kueleeza changamoto mbali mbali za maradhi yanayowakabili na
kuchunguzwa na hatiame kupata dawa na ushauri wa kitaalamu.
Katika hafla hiyo Mke wa Balozi wa China aliopo nchini Bi Liu Jie aliikabidhi
zawadi na vifaa mbali mbali kwa wazee wanaoishi nyumba za wazee
Welezo na Sebleni.
Nyumba za kutunzia wazee ziliopo Welezo na Sebleni zina jumla ya
wazee 71 wa kike na kiume, ambao hupatiwa huduma zote muhimu,
ikiwemo Chakula, malazi, matibabu na Serikali.