Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimsikiliza Mkuu wa Gereza Kitai, Kamishna Msaidizi wa Magereza,Dkt. Sylivesta Shija baada ya kukagua miundo mbinu ya bwawa litakalotumika kwa Kilimo cha Umwagiliaji katika shamba la Gereza Kitai ili kuondokana na tatizo la ukame linalosababisha kuporomoka kwa mazao.Naibu Waziri yuko mkoani Ruvuma kutembelea shamba hilo ambalo ni moja kati ya mashamba kumi ya magereza nchini yaliyoteuliwa kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka magereza yajitosheleze kwa chakula cha wafungwa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza baada ya kufika katika Gereza la Kitai.Naibu Waziri yuko mkoani Ruvuma kutembelea shamba la gereza hilo ambalo ni moja kati ya mashamba kumi ya magereza nchini yaliyoteuliwa kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka magereza yajitosheleze kwa chakula cha wafungwa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikagua miundo mbinu ya bwawa litakalotumika kwa Kilimo cha Umwagiliaji katika shamba la Gereza Kitai ili kuondokana na tatizo la ukame linalosababisha kuporomoka kwa mazao.Naibu Waziri yuko mkoani Ruvuma kutembelea shamba hilo ambalo ni moja kati ya mashamba kumi ya magereza nchini yaliyoteuliwa kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka magereza yajitosheleze kwa chakula cha wafungwa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Sajenti Patrick Mmela akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ya mtambo wa kufulia umeme uliokuwa ukitumika katika bwawa lililopo Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai ambalo jeshi la magereza wameelekezwa kulitumia bwawa hilo kwa kilimo cha umwagiliaji ili kuondokana na tatizo la ukame katika mashamba ya gereza hilo ambalo ni moja kati ya magereza kumi nchini yaliyopo katika mkakati wa kulisha wafungwa. Naibu Waziri yuko mkoani Ruvuma kutembelea gereza hilo ambalo ni moja kati ya magereza kumi nchini yaliyoteuliwa kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka magereza yajitosheleze kwa chakula cha wafungwa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Uongozi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Songea baada ya kukagua shehena ya mahindi iliyohifadhiwa katika Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai.Naibu Waziri yuko mkoani Ruvuma kutembelea gereza hilo ambalo ni moja kati ya magereza kumi nchini yaliyoteuliwa kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka magereza yajitosheleze kwa chakula cha wafungwa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi