**********************************
Ahmed Mahmoud/Arusha
Naibu Ktibu Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imedhamiria kuwa na VISA moja kwa lengo la kupunguza urasimu ndani ya Jumuiya hiyo
Hayo yameelezwa leo na Naibu Mtendaji Mkuu wa SADC Dkt Thembinkosi Mhilongo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa wenye dhamana na Wizara za Maingira,Maliasi na Utalii katika nchi hiyo za Ukanda wa Kusini mwa bara la Afrika za SADC
Dkt Mhilongo pia amesema nchi za SADC zimejipanga kuangalia kwa kina suala la Viumbe na Mimea Vamizi katika nchi hizi wananchama za SADC pamoja na Wanyama ambao wakati katika hatari ya kutoweka katika nchi hizi
Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri hao wenye dhamana hii ya mazingira, maliasili na utalii kuhakikisha wanangalia kwa kina Itifaki na Mikataba inayohusu Sekta hizi tatu katika nchi Wanachama za SADC
Amesema Mkutano wa Mawaziri haw ani muhimu katika kukuza na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa mataifa ya SADC.
Hivyo amewataka wakati wa Mkutano huo wanapaswa kupima na kuangalia kwa kina Sera na Itifaki zinazosimamia Sekta hizi tau ambazo ndio muhimili mkuu wa Uchumi wa mapataifa haya
Mbali na kungalia masuala hayo Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC amewataka Mawaziri hao kuhakikisha wanangalia kwa Kina Hima Sheri azote zinazosimamia na kuongoza Sekta hizi katika Jumuiya hii. Amesisitiza Naibu Mtendaji Mkuu huyo wa SADC Dkt Mhilongo
Amesisitiza kuangaliwa upya Itifaki ya Utalii, Mazingira, na Maasili katika nchi Wanachama za SADC na mbadiliko ya tabianchi
Amesisitiza umuhimu kwa Mawaziri hao kuhakikisha majandiliano ya Mkutano wao yalenge katika kutatua changamoto zinazokabili sekta ya mazingira, maliasili na Utalii katika nchi za SADC
Ameeleza kwamba mkutano wa mwisho kufanyika kwa Mawaziri wa SADC ulifanyika Novemba 2017 Mjini Pretoria Afrika ya Kusini
Nchi za SADC imebahatika kuwa na raslimali lukuki zikiwemo zaWanyamapori, misitu, Uvuvi raslimali ambazo ni muhimu katika kuchangia ukuaji wa Uchumi na maendeleo ya nchi wanachama za SADC.Amesisitiza Dkt Mhilongo
Mabadiliko ya tabianchi yanazidi kuathiri mataifa haya ya kusini mwa Afrika na kuathiri hali ya uzalishaji katika Sekta za Kilimo, ufugaji na maendeleo ya ukanda huu.Amesisitiza Dkt Mhilongo
Amewataka Mawaziri hao kuangalia kwa kinja Itifaki ya SADC inayohusu umuhimu wa kusimamia na kulinda uhifadhi, kuangalia Itifaki ya misitu, Uvuvi na Sheria ya usimamizi wa Wanyamapori
Pia amesisitiza umuhimu kwa SADC Kutambua umuhimu wa kusimamia , kulinda na kuhifadhi misitu ili kuwa na uhifadhi endelevu katika nchi hizi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika
Naibu Mtendaji Mkuu huyo amesema Jiji na Mkoa wa Arusha limebeba historia kubwa ya SADC kutokana na kuwa Jiji hili ndipo chimbo kubwa la kuanzishwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika miaka 40 iliyopita
Amesema SADC iliasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Keneth Kaunda wa Zambia, Rais Somora Machel wa Msumboji na Rais Austino Neto wa Angola na Rasi Gabriel Mugabe wa Zimbabwe ambapo Jumuiya hiyi iliasisiwa katika Ukumbi huo wa AICC
Aidha Mkataba wake ulisainiwa Lusaka Nchini Zambia kwa ajili ya kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ambapo Makao ya SADC yapo Gabron Botswana
Aidha kukosekana kwa Visa moja kwa Watalii ulaya wanapokuja katika ukanda huu wa kusini mswa nchi za kusini mwa Afrika ni moja ya changamoto kubwa