Home Mchanganyiko WATAALAM SEKTA YA MAENDELEO NCHINI WATAKIWA KUWA NA MFUMO MAALUM WA KUPATA...

WATAALAM SEKTA YA MAENDELEO NCHINI WATAKIWA KUWA NA MFUMO MAALUM WA KUPATA TAKWIMU

0

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua mwongozo wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini mara baada ya kufungua Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kushoto kwake ni Rais wa wa CODEPATA Bw. Sunday Wambura na kulia kwake ni Bw. Patrick Golwike Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara yake.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa hotuba yake kwa Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua chama cha wataalam wa maendeleo ya jamii nchini CODEPATA mara baada ya kufungua Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea zawadi iliyotolewa kwake na chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini CODEPATA mara baada ya kufungua Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua banda la Wizara yake mara baada ya kufungua Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.

Baadhi ya Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wakifuatailia jambo kwa umakini wakati wa  Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

……………..

Na Mwandishi Wetu Dodoma

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini kujiongeza katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanakuwa na takwimu sahihi za matukio ya ukatili badala ya kutegemea taarifa za Jeshi la Polisi ambazo utolewa na Mkuu wa Jeshi hilo baada ya mwaka mzima.

Waziri Ummy amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wataalam wa maendeleo ya Jamii linaloendelea kwa siku mbili kama sehemu ya Mkutano Mkuu wa mwaka wa wataalam wa maendeleo ya jamii.

Waziri Ummy amesema wataalam wenzao wa afya wamekuwa wakimpatia taarifa zenye takwimu kwa wakati na kuwataka wataalam hao kuiga mfano huo kwa kuwataka kuwa wanawasiliana na vituo vya polisi mkoani kwao ili waweze kupata taarifa za waanga wa ukatili katika maeneo yao kazi.

“Kila nikienda katika ziara sipewi taarifa yoyote kutoka kwa wataalam wa maendeleo ya jamii na hata nikiwauliza unakuta hawana taarifa yoyote ile kuhusina na masuala yanayohusiana na masuala ya Maendeleo ya Jamii.’’ Aliongeza Waziri Ummy.

Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy amemwagiza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Nchini Bw. Patrick Golwike kuweka mfumo mzuri wa kukusanya takwimu za maendeleo ya jamii ili kuwezesha kupatikana kwa takwimu izo kwa muda na kwa haraka.

‘’Nikija katika Mkoa au Halmashauri yako nipate takwimu, ukiongea na takwimu ni rahisi kupata rasilimali fedha na misaada mingine itakayosaidia kutatua changamoto zilizopo mfano kupata takwimu za vikundi vya wajasiliamali ambao wamepokea mikopo ya Halmashauri’’. Aliongeza Waziri Ummy.

Pamoja na kutoa changamoto hizo kwa wataalam hao Waziri Ummy amewataka wataalam hao kuhamasisha jamii ili iweze kutumia teknolojia ya habari kwa ajili ya kujiletea maendeleo na kuongeza kuwa kwa kutumia taarifa zinazopatikana jamii itapata taarifa za masoko ya bidhaa zao ikiwemo namna bora ya kulima kwa utaalam.

Aidha Waziri Ummy ameitaka jamii kuacha kutumia muda mwingi kufuatilia mitandao ya kijamii na badala yake wahamasishwe kutumia muda wao mwingi kwa mambo yenye tija ikiwemo ari ya kuchangia jamii kwa ajili ya maendeleo.

Waziri Ummy ameitaka jamii ya watanzania kuwa  inapenda starehe sana na watu wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya kusherekea harusi, siku ya kuzaliwa bila kujiuliza kama fedha hizo zinaendana vipaumbele ambavyo mtu amejiwekea au kuchangia ada kwa ajili ya mwanafunzi. 

Waziri ummy ameitaka jamii kutumia teknolojia hiyo kufanya mambo yenye tija na akitoa mfano wa wataalam wa maendeleo ya jamii kuendelea kuhamasisha jamii kuwekeza katika elimu ya Afya ili tuweze kupata huduma bora katika jamii.

Aidha amewataka wataalam hao kufikilia kuwekeza sana katika miradi ambayo ina mashiko na kukemea tabia ya wafadhili kuweka mkazo katika masuala ya warsha na Semina ambazo hazitoi matokeo ya moja kwa moja katika jamii.

Akizungumza kwa Niaba ya katibu Mkuu Maendeleo ya jamii, Mkurugenzi wa maendeleo ya Jamii bw.Patrick Golwike amseme ajukuu kubwa la wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni kuiandaa jamii ushiriki katika shughuli za maendeelo ya nchi.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Bw. Sunday Wambura amesmea kuwa Mkutano Mkuu wa mwaka huu umekuja na uzinduzi wa Chama chao kitakachowasaidia kupeana mbinu mbalimblia za kuhakikisha maafisa wanaisaidia jamii katika kujiletea maendeleo.

Wataalamu wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii wanakutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne.