Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Adadi Rajabu (katikati) akieleza jambo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kituo cha Taifa cha kuhifadhi taarifa (NIDC) ambacho kipo chini ya usimamizi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Isack Kamwelwe, Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Waziri Kindamba na wengine ni Wajumbe wa Kamati hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Isack Kamwelwe akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kujionea uendeshaji wa Shirika hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Waziri Kindamba akielezea jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kujionea uendeshaji wa Shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Mohammed Khamis Omar akielezea jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kituo cha Taifa cha kuhifadhi taarifa (NIDC).
Mbunge wa Buhigwe na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Albert Ntabaliba akichangia jambo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kituo cha Taifa cha kuhifadhi taarifa (NIDC).
PICHA NA BUNGE