Home Biashara CRDB yatumia AALCO kujitangaza

CRDB yatumia AALCO kujitangaza

0
Na Suleiman Msuya
BENKI ya CRDB ambayo ni mdhamini wa Mkutano Mkuu wa 58 wa mwaka wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria ya nchi
za Afrika na Asia (AALCO) imesema itautumia mkutano huo kujitanga na kutanua soko la biashara.

 

Hayo yamesemwa na
Meneja Mwandamizi Idara ya Serikali za Mitaa CRDB, Suzan Shuma, wakati
akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC) jijini Dar es Salaam ambapo mkutano huo unafanyika.

 

Shuma alisema benki
hiyo inatembea na kauli mbiu yao ya ulipo tupo hivyo inaamini ushiriki wake
katika mkutano huo wataweza kujitangaza kwa nchi shiriki.

 

Alisema kwa sasa CRDB
inapatikana Tanzania na nchini Burundi hivyo ni wazi kuwa siku chache zijazo
wataweza kufikia nchi nyingine.

 

“Benki ya CRDB ni mdau
mkubwa wa maendeleo ambapo inashiriki miradi mingi ya Serikali hivyo kupitia
mkutano huu wa AALCO tunatarajia kujitangaza zaidi kibiashara,” alisema.

 

Shuma alisema katika
mkutano huo wa AALCO benki hiyo itakuwa inatoa huduma ya kutoa na kubadilisha
fedha na kutoa kadi.

 

Alisema mikakati ya
benki hiyo ni kuendelea kuwa kinara wa kutoa huduma za kibenki nchini na nje ya
nchi.

 

Akizungumza katika
mkutano huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome
alisema CCDB ni moja ya wadhamini wa mkutano huo.

 

Alisema Serikali
inaipongeza benki hiyo kujitokeza kudhamini mkutano huo na kwamba haijakosea
kufanya hivyo kwa kuwa mkutano huo ni fursa ya kujitangaza kimataifa.

 

Mkutano wa AALCO
unashirikisha nchi 49 za Bara la Asia na Afrika ambapo viongozi katika Sekta ya
Sheria hukutana na kujadiliana namna ya kutatua changamoto za kisheria na haki
za kibinadamu kwenye nchi wanachama.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akifungua rasmi Mkutano wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO), jijini Dar es Salaam Oktoba 21, 2019, mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya CRDB.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, akitoa hotuba yake wakati wa Mkutano wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO), jijini Dar es Salaam Oktoba 21, 2019, mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya CRDB.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 58 wa Mwaka wa Shirika la Mashauriano ya Kisheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO) uliofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 21, 2019, mkutano huo umedhaminiwa na Benki ya CRDB.

Washiriki wa mkutano.

Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.

Washiriki.
Meneja Mwandamizi anayeshughulikia Idara Kitengo cha Biashara ya Serikali Benki ya CRDB, Suzan Shuma (wa pili kulia) akifuatilia mkutano huo pamoja na wafanyakazi wenzake.
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Rais wa AALCO kwa sasa, Augustine Mahiga, akizungumza katika mkutano huo.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa mkutano huo Benki ya CRDB.

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Rais wa AALCO kwa sasa, Augustine Mahiga, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki ya CRDB.

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Rais wa AALCO kwa sasa, Augustine Mahiga, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mwandamizi anayeshughulikia Idara za Serikali za Mitaa wa Benki ya CRDB, Suzan Shuma.

Meneja Mwandamizi Benki ya CRDB, anayeshughulikia Idara za Serikali za Mitaa, Suzan Shuma, akizungumza na waandishi wa habari.