NJOMBE
Watuhumiwa wawili wa kesi ya kujeruhi akiwemo Milton Wikunge(56)ambaye ni mchungaji wa kanisa la Baptisti na mkazi wa kijiji cha Mawindi pamoja na Nolbat Mbude mkazi wa Igima wilayani Wanging’ombe mkaoni Njombe wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe leo octoba 21 kujibu mashtaka ya tuhuma tatu za kujeruhi waumini watatu katika kanisa hilo.
Akisoma mastaka yanayowakabili watuhumiwa hao mwendesha mashtaka wa serikali Hapness Makungu amesema watuhumiwa wanakabiliwa na makosa matatu ya kujeruhi kinyume na Kifungu cha sheria 225 cha seria ya kanuni ya adhabu kifungu no 16 marejeo ya 2002 ambayo waliyafanya octoba 13 kwa watu watatu ambao wadaiwa kuwa ni waumini wa kanisa hilo ambao ni Elesi Fwami,Shahibu Mhema na Regina Lyahumi.
Watuhumiwa wote wamekana kuhusika na tuhuma hizo za kujeruhi jambo ambalo limefanya mahakama kupitia kwa hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe Iluvan Msaki kuahirisha kesi hiyo hadi octoba 31 itakapotajwa tena kwa lengo la kuendelea na uchunguzi zaidi.
Fullshangwe imezungumza na mkuu wa wilaya ya Wangingombe Comrade Ally Kassinge anakiri kutokea kwa matukio hayo ambapo amesema kwa taarifa za awali inaonyesha watuhumiwa walitoa adhabu ya viboko kwa waumini hao kwa lengo la kuwapa toba ya makosa waliyatenda na kuwasabishia majeraha makubwa kwa muumini anaetambulika kwa jina la Elisia Fwime ambaye amelazwa hospitali ya Kibena wilayani Njombe .
Kufuatia hali hiyo mkuu huyo wa wilaya anasema amejipanga kufanya ziara wilaya nzima kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kupinga vitendo vya imani potofu ikiwemo ya kanisa linalotuhumiwa kuwaadhibu waumini wao ili kutubu dhambi zao.
Watuhumiwa wote wawili ambao ni viongozi wa kanisa hilo walitiwa nguvuni na vyombo vya dora baada ya kukutwa na tuhuma za kuwaadhibu waumini wao watatu viboko na kusababisha majeraha makubwa kwa lengo la kuwapa toba jambo ambalo limepingwa vikali na serikali wilayani humo.
Katika hatua nyingine watumiwa hao wameshindwa kupata dhamana ambayo inagharimu mil 3 kutokana na wadhamini wao kukosa barua kutoka kwa mtendaji wa kata.