Home Mchanganyiko MKUTANO WA WATAALAM MAENDELEO JAMII WAAHIRISHWA HADI OKTOBA 21,2019

MKUTANO WA WATAALAM MAENDELEO JAMII WAAHIRISHWA HADI OKTOBA 21,2019

0

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mkutano wa 14 wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii uliopangwa kufanyika kesho jijini Dodoma, umeahirishwa hadi Oktoba 21-24, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Patrick Golwike, amesema mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya jamii(CODEPATA), lakini umesongezwa mbele kutokana na sababu zisizozuilika.

“Mkutano huu ambao ulikuwa wa 14 ulipangwa kufanyika Dodoma kuanzia Oktoba 8-11, mwaka huu, lakini mkutano huu umesogezwa mbele kutokana na sababu zisizozuilika na utafanyika kuanzia Oktoba 21—24, mwaka huu.Wizara inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza,tunafahamu wapo watu safarini na wengine wameshafika Dodoma,”amesema.

Ameeleza kuwa mwaka 2001 Wizara imekuwa ikifanya mkutano mkuu wa wataalam hao kwa lengo la kubadilishana uzoefu na utendaji kazi na kutekeleza majukumu ya sekta.

“Hadi sasa mikutano 13 imeshafanyika na kuhudhuriwa na wataalam wa kada ya maendeleo ya jamii kutoka sekretarieti za mikoa, mamlaka za serikali za mitaa, taasisi za wizara na wizara za kisekta pamoja na asasi za kiraia na mkutano wa 13 ulifanyika Arusha Septemba 23-29, mwaka jana ambapo uliongeza wigo wa ushiriki,”amesema.