Home Mchanganyiko MATUKIO MBALIMBALI KWENYE ZIARA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI...

MATUKIO MBALIMBALI KWENYE ZIARA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI KATIKA MAONESHO YA TEKNOLOJIA NA UWEKEZAJI WA MADINI GEITA TAREHE 23 SEPTEMBA, 2019

0

Mtaalam kutoka Tume ya Madini, Monica Mkumbo (kulia) akielezea majukumu ya Tume ya Madini kwa mchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Kakola mkoani Geita, Yohana James (kushoto) kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 23 Septemba, 2019.

Fundi Sanifu Migodi Mwandamizi, Msafiri Kussa na Mjiolojia Asimwe Kafrika kutoka Tume ya Madini wakitoa elimu kwa umma kwa wanafunzi wa shule za msingi za Kalangala na Nyasa waliotembelea banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 23 Septemba, 2019.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili katika banda la Tume ya Madini, kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 23 Septemba, 2019.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 23 Septemba, 2019.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji wa Madini yanayoendelea mjini Geita tarehe 23 Septemba, 2019.