Home Mchanganyiko WAZIRI HASUNGA APIGA MARUFUKU KUFUNGA MIPAKA YA UUZAJI MAZAO

WAZIRI HASUNGA APIGA MARUFUKU KUFUNGA MIPAKA YA UUZAJI MAZAO

0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika katika ofisi ndogo Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika katika ofisi ndogo Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Septemba 2019.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika katika ofisi ndogo Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Septemba 2019.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika katika ofisi ndogo Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Septemba 2019.

 

Sehemu ya watumsihi wa Wizara ya Kilimo wakifuatilia kikao kazi hicho wakati wa mkutano ulioitishwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) katika katika ofisi ndogo Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Septemba 2019.
 
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Dodoma
 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema
kuwa serikali haikusudii kufunga mipaka ya uuzaji wa mazao hivyo
wafanyabiashara wana ruksa ya kuuza mazao popote watakapo.
 
Mhe Hasunga ameyasema leo tarehe 13 Septemba 2019 wakati
akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika katika ofisi ndogo Jijini
Dodoma.
 
Waziri Hasunga amesema kuwa wizara hiyo haitapiga marufuku usafirishaji na uuzaji wa mazao ya
kilimo nje ya nchi na haina mpango wa kuweka katazo hilo ili kuongeza wigo wa
upatikanaji wa soko la wakulima kwa kuwa Taifa lina chakula cha kutosha.
 
Mhe Hasunga, ametoa wito kwa wakulima
na wafanya biashara wanaojishughulisha na kununua au kuuza mazao ya kilimo
kuendelea na biashara yao  ili kuongeza tija kwa wakulima.
Aidha, amewataka wakulima kuendelea
kuchangamkia fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi ambazo zina upungufu au
uhitaji wa mazao hayo.

Alisema kuwa jukumu kubwa la serikali ni kuhakikisha kwamba taifa
linajitosheleza kwa chakula na kilimo kinaendelea kutoa ajira kwa watanzania
walio wengi.
 
“Wakati mkulima anahangaika na kilimo mlishirikiana
nae, wakati anahangaika kulima mlimpelekea pembejeo, wakati anavuna
mlishirikiana nae, lakini sahizi mnataka kuleta masharti ya nini” Alihoji Mhe
Hasunga
 
Awali akizungumza kwenye mkutano huo Naibu Waziri
wa Kilimo Mhe Omary Mgumba amesema kuwa ili kilimo kiwe
na tija ni lazima serikali ijikite katika miundombinu ya barabara hasa vijijini
ili mazao ya wakulima yaweze kufika sokoni kwa wakati hiyo ndiyo sababu ya
bajeti ya serikali kujikita katika kujenga miundombinu ya barabara.
Hata hivyo amewataka wafanyakazi wa
serikali na wizara ya kilimo kufanya kazi zenye viwango bila kuangalia kiwango
cha mshahara wanaolipwa kwani baada ya serikali kuyafanya maendeleo mishahara
itapandishwa.
Aidha, ameongeza kuwa vijana
waliopelekwa Israeli kwa ajili ya mafunzo itakuwa vyema kama watapelekwa kwenye
Halmashauri au kwa wakulima kwa ajili ya kwenda kuonyesha kwa vitendo teknolojia
walizo jifunza kwa kuwasaidia  wakulima kuboresha kilimo chao.
Naya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein
Bashe amewataka watendaji hao kuongeza tija na uzalishaji katika kilimo kwani
kwa sasa serikali imejipanga katika kukuza sekta ya viwanda hivyo ni lazima
mazao ya kilimo yatakayo hitajika yawe yana ubora na yakutosha.
Alisema kuwa watendaji hao hawapaswi
kuangalia upungufu wa vifaa na miundombinu ya kufanyia kazi badala yake wanapaswa
kuongeza juhudi kuhakikisha kuwa wanaandaa vitu vyenye ubora.
“Waziri hawezi
kwenda kwa Dokta Mpango kuomba hela kwa ajili ya kuwekeza kwenye eneo fulani
hata pata kama ubora wa kile kitu hauonekani” Alisisitiza Mhe Bashe