Home Mchanganyiko Ni Muhimu kwa lugha kuwa na kanuni Zake, Dkt. Mwakyembe

Ni Muhimu kwa lugha kuwa na kanuni Zake, Dkt. Mwakyembe

0

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akionyesha kitabu cha Kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa mara baada ya kuzindua leo Jijini Arusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza jambo mara baada ya kuzindua kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa  leo Jijini Arusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa bao Bwana Twaha Mohamed (kushoto)  katika hafla ya uzinduzi wa kanuni za Baraza la Kiswahili la Taifa leo Jijini Arusha.

 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  akizungumza na wajasiliamali wa kazi za sanaa za ufundi alipotembelea banda hilo  leo Jijini Arusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewange (kulia) alipotembelea banda la uchapishaji wa vitabu la Mkuki (Mkuki Publishers) leo Jijini Arusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Kiswahili la Taifa mara baada ya kuzindua  kanuni za Baraza hilo leo Jijini Arusha.

(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha)

……………………

Na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa ni muhimu kwa lugha  ya Kiswahili kuwa na kanuni ambazo zitasaidia katika kufanikisha mawasiliano kwa jamii ili kuleta maendeleo chanya.

Hayo aliyasema leo Jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa kanuni  za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) lengo ikiwa ni kuwazesha  kusimamia matumizi ya lugha.

“Ni muhimu kwa kila lugha kuwa na kanuni  na sifa kubwa ya lugha ya Kiswahili ni unyumbulifu, hivyo ninaamini kupitia kanuni hizi tutakuwa na usimamizi mzuri wa matumizi ya lugha hii” Dkt. Mwakyembe

Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa lazima kanuni hizo ziwe nyumbulifu na rafiki ili kuweza kuzifanyia marekebisho endapo kutakuwa na mapungufu yoyote wakati wa utekelezaji wake.

Pia aliwapongeza wataalamu wote kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali walioweza kufanikisha upatikanaji wa kanuni hizo na kuwataka kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kukuza, na kuendeleza  lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewange alilezea kuwa kuzinduliwa kwa kanuni hizo ni mojawapo ya mafanikio makubwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Leo tunaweka historia nzuri katika nchi yetu kwa hatua hii muhimu ya kufanikisha uzinduzi wa kanuni za lugha ya Kiswahili ambazo pia zinatupa fursa ya kuwa na marekebisho kwa kadri zitakavyokuwa zinatekelezwa” Dkt. Sewange.

Historia inaeleza kuwa Baraza la Kiswahili la Taifa liliundwa na sheria ya bunge Na. 27 ya mwaka 1967 kwa shabaha ya kukuza, kuimarisha na kuendeleza Kiswahili  nchini na baadaye kufanyiwa marekebisho mwaka 1983 kwa sheria ya Bunge Na. 7 ikiwa imepewa uwezo wa kufuatilia na kusaidia ukuzaji wa Kiswahili nje ya nchi na baadaye  sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho ya mwisho mwaka 2016.