Home Burudani Katibu Mkuu Bibi Susan Mlawi awapongeza washiriki wa Multichoice Talent Facotry Academy...

Katibu Mkuu Bibi Susan Mlawi awapongeza washiriki wa Multichoice Talent Facotry Academy kwa kuiwakilisha vyema Nchi.

0

Meneja Biashara kutoka Kampuni ya Multichoice Bw.Jonson Mshana (kulia)
akitoa maelezo mafupi kuhusu “Multichioce Talent Factory Academy” iliyodhamini
vijana wanne katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmoja
yaliyoandaliwa na Kampuni hiyo Nchini Kenya walipofika ofisi ya Katibu Mkuu
Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi (kulia) kuelezea
namna walivyonufaika na mafunzo hayo.

Jamal Mohamed Kishuli ambaye ni miongoni mwa Vijana wanne
waliorejea kutoka nchini Kenya walikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu
kwa mwaka mmoja yaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati
lijulikanalo kama “Multichioce Talent Factory Academy” akizumngumza wakati
walipomtembelea Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi
Susan Mlawi ofisini kwake Jijini Dodoma.

Bw.Wilson Nkya miongoni mwa Vijana wanne waliorejea kutoka nchini Kenya
walikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmoja
yaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati lijulikanalo kama
“Multichioce Talent Factory Academy” akizumngumza wakati walipomtembelea
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi
(hayupo katika picha) ofisini kwake Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Susan Mlawi
akiwa katika picha ya pamoja na Vijana waliorejea kutoka nchini Kenya
walikokuwa katika mafunzo ya uandaaji wa filamu kwa mwaka mmoja
yaliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice chini ya dawati lijulikanalo kama
“Multichioce Talent Factory Academy” baada ya kupokea taarifa ya mafunzo
waliyopata walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma.

******************

Na Shamimu Nyaki – WHUSM

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi.Susan Mlawi
amewapongeza vijana wanne waliofanya vizuri katika mafunzo ya uaandaaji wa
Filamu yalioandaliwa na Kampuni ya Multichoice yaliyofanyika nchini Kenya
ambapo amewataka kutumia taaluma waliyopata kutengeneza filamu bora zenye
maudhui ya kuitangaza nchi yetu na kuleta ushindani katika soko.

Katibu Mkuu Bibi. Susan ameyasema hayo leo ofisini kwake Jijini Dodoma baada ya
kutembelewa na vijana hao ambao amewataka kufika katika Bodi ya Filamu
Tanzania kuwasilisha uelewa waliopata na kushauri namna ambavyo Bodi hiyo
inaweza kuwatumia katika tasnia hiyo.

“Nawapongeza sana kwa kufanya vizuri katika mafunzo mliopewa,naamini
mtayatumia vizuri katika kukuza vipaji vyenu na kusaidia mawazo kwa wengine
ambao hawajapata nafasi hii,Lakini pia mtatumia ujuzi na taaluma mliyopata
katika kuleta mapinduzi ya utengenezaji wa filamu hapa nchini”alisema Bibi Susan.

Naye Meneja wa masuala ya Biashara wa Kampuni ya Multichoice Bw.Jonson
Mshana amesema kuwa Kampuni hiyo imeanzisha dawati la kusaka vipaji vya
uandaaji wa kazi za filamu (Multichoice talent Factory Academy) kwa Bara la
Afrika ili vijana wenye uwezo na vipaji kupata fursa ya kuongezewa maarifa
pamoja na kutafuta ajira kwa njia rahisi.

Bw.Jonson ameongeza kuwa Kampuni hiyo kila mwaka inatafuta vijana wanne
ambao wanapatikana kwa kuomba nafasi hiyo na hatimaye kufanyiwa usaili na
kujiunga na wenzao kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Kenya,Ethiopia,
Uganda na Nigeria.

Naye Kijana Jamal Mohamed Kishuli ambaye amejifunza “Art Designer” amesema
kuwa vijana wanapaswa kujiamini katika kila wanachokifanya na kutokata tamaa
lakini pia zinapotokea fursa za kuonyesha uwezo wao basi wasisite kujitokeza ili
kupata nafasi ya kujitangaza kupitia vipaji walivyonayo.

Vijana hao walikua katika mafunzo ya Uandishi wa Mswada (Script Writer),
Uandaaji (producer) Uongozaji (Directing) na Art Desgner ambayo wamejifunza
kwa mwaka mmoja katika Chuo Kikuu cha Kenyata nchini Kenya.