Home Mchanganyiko UTIAJI SAINI WA MUENDELEZO WA UJENZI WA MAABARA YA TAEC AWAMU ...

UTIAJI SAINI WA MUENDELEZO WA UJENZI WA MAABARA YA TAEC AWAMU YA PILI

0

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) Profesa Lazaro Busagala akibadilishana mktaba wa muendelezo wa ujenzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa maabara ya TAEC, ujenzi wenye thamani ya shilingi Bilioni 10,447,749,433.24 na Mkurugenzi wa Kampuni ya M/S LI JUN DEVELOPMENT COMPANY LTD. maabara hiyo itajengwa kwenye makao makuu ya TAEC yaliyopo Njiro jijini Arusha.

*****************************

Arusha, 10 Septmba 2019

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imesaini mkataba wa shilingi
bilioni 10,447,749,423.24 na kampuni ya ujenzi ya M/S LI JUN
DEVELOPMENT CONSTRUCTION LTD kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili
maabara ya kisasa.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) Profesa
Lazaro Busagala ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha inajenga maabara hiyo kwa
kiwango cha hali ya juu kulingana na makubaliano ya mkataba husika.

Maabara hiyo ni mwendelezo wa maabara ya awamu ya kwanza iliyozinduliwa
mwezi April mwaka huu na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa. Ujenzi huu wa maabara ni juhudi zingine za
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli
katika kuendelea kuleta maendeleo nchini.