Home Burudani BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA AFURAHIA ONESHO LA MCHANGO WA MWALIMU NYERERE...

BALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA AFURAHIA ONESHO LA MCHANGO WA MWALIMU NYERERE KATIKA UKOMBOZI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA

0

Balozi wa Norway nchini Tanzaia, Mhe. Elizabeth Jacobsen (wa pili kutoka kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa Makumbusho, Bibi Flora Vicent  juu ya mchango wa Mwalimu J.K. Nyerere katika Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika alipotembelea Makumbusho ya Taifa leo. Anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Gwakisa Kamatula na kulia kwake ni Wilbard Lema Mhifadhi, Makumbusho ya Taifa

Balozi wa Norway nchini Tanzania akifurahia pikipiki aliyotembelea Rais wa Zamani wa Msumbiji, Hayati Samola Machel wakati wa mapambano ya kupigania uhuru wa  nchi yake. Pikipiki hiyo ipo katika maonesho ya Mchango wa Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere katika Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika yaliyopo Makumbusho ya Taifa. Kushoto kwake ni Bibi Flora Vicent Mhifadhi, Makumbusho ya Taifa.

Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe.Elizabeth Jacobsen akipata maelezo kutoka kwa Bibi Flora Vicent, Mhifadhi, Makumbusho ya Taifa juu ya machine iliyokuwa ikitumika kutoa mafunzo ya afya wakati wa vita vya kupigania uhuru wa nchi za Kusini mwa Afirka alipotembelea onesho la Mchango wa Mwalimu J.K. Nyerere katika Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika leo. Nyuma ni Afisa Elimu Bibi Magreth Kigadye

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt Gwakisa Kamatula akifurahia jambo akiwa na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe, Elizabeth Jacobsen alipotembelea onesho la Mchango wa Mwalimu J.K. Nyerere katika Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika leo. Kushoto kwa Kaimu Mkurugenzi ni Afisa Elimu Bibi Magreth Kigadye