MKURUGENZI wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Suphian Baruani amesema mtoto Anisia, pacha aliyetenganishwa na mwenzake baada ya kuzaliwa wakiwa wameungana na kupelekwa Saudi Arabia kutenganishwa, amefariki Dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zikiwa zimepita siku chache tangu waliporejea nchini wakitoka Saudi Arabia walikofanyiwa upasuaji.