Home Mchanganyiko MKUTANO WA 50 WA MABUNGE YA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA KANDA...

MKUTANO WA 50 WA MABUNGE YA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA

0

BAADHI ya Wajumbe wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola  kwa Kanda ya Afrika wakiwa katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar uliofunguliwa leo rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo  pichani).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola  kwa Kanda ya Afrika  leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola  kwa Kanda ya Afrika leo  unaofanyika  katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola  kwa Kanda ya Afrika  leo unaofanyika  katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar

BAADHI ya Wajumbe wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola  kwa Kanda ya Afrika   katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar  wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo  pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake ya   ufunguzi rasmi wa Mkutano  huo unaofanyika Hotelini hapo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola  kwa Kanda ya Afrika  leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Job Ndugai na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Zubeir Ali Maulid na Spika wa Bunge la Kenya pia Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Chama cha Mabunge  Justin Maturi (katikati) wakiongozwa na Mpambe Mwinyi Haji Abu(mwenye Siwa) wakati  leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo  pichani) akiingia katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kufungua Mkutano wa 50  wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola  kwa Kanda ya Afrika 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Spika wa Mabunge wa Nchi mbali mbali wakisimama wakati Wimbo wa Taifa wa Ukipigwa katika  ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola  kwa Kanda ya Afrika  uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Job Ndugai (kulia)  Spika wa Bunge la Kenya pia Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji Chama cha Mabunge  Justin Moturi (katikati) Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Zubeir Ali Maulid (wa pili kushoto)  na Spika wa Bunge la Uganda Rebecca  Alitwala  Kadaga  wakisimama wakati Wimbo wa Taifa wa Ukipigwa katika  ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola  kwa Kanda ya Afrika  uliofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahar Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Picha na Ikulu

………………

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kwamba teknolojia ya habari na mawasiliano ina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko ya maendeleo katika Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola.

Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Chama Cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinatul Bahr, iliyopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Rais Dk. Shein alisema kwamba iwapo teknolojia ya habari na mawasiliano itatumika ipasavyo hasa katika kuimarisha kanzi data mbali mbali hatua hiyo itarahisisha suala zima la kufanya maamuzi kwa wakati na kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa.

Aliongeza kuwa uendeshaji wa Bunge kwa kutumia njia za kisasa kunawaweka karibu zaidi Wabunge na wananchi, jambo ambalo linatoa fursa pana zaidi kwa wananchi ya ya kutoa maoni yao na hoja mbali mbali za maendeleo zinazogusa maisha yao ya kila siku.

Alieleza kuwa Bunge Mtandao ni nyenzo nzima ya kupunguza harama za mambo mbali mbali kama vile usafiri sambamba na kuokoa muda.