Home Mchanganyiko “ADHABU ZA SHULENI NI ADHABU ZA UPENDO”;PADRI JISO

“ADHABU ZA SHULENI NI ADHABU ZA UPENDO”;PADRI JISO

0

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
“ADHABU
mnazopewa shuleni ni adhabu za upendo, zinalenga kuwarekebisha ili akili ziweze
kupokea maarifa mnayopewa na walimu na hatimaye muwe raia wema wenye uwezo wa kuztumikia
taifa na jamii, tofauti na adhabu mtakazopewa baada ya kumaliza elimu, huko mitaani
mtakutana na adhabu za chuki zinazotokana na maarifa kidogo mliyonayo.” Hayo ni
maneno yaliyosemwa na Padri Jiso kutoka Mtakatifu Vincent wakati wa mahafali ya saba ya darasa
la saba shule ya Carmel Convent
iliyoko Vikindu, Wilayani Mkuranga

Padri Jiso ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafaki hayo ambayo ni ya saba
kufabyika katika shule hiyo, aliwaasa wanafunzi kuendeleza yale mema
waliyojifunza katika kipindi cha miama saba waliyokuwa shuleni.
Alisema
binadamu wametunukiwa zawadi kubwa na Mwenyezimungu ya kutumia maarifa na akili
katika kuyatawala mazingira, licha ya kwamba sayansi inaonyesha miaka mingi ya
nyuma binadamu ambaye yuko katika kundi la wanayama, na kama walivyo wanayama
wengine aliishi porini.
 “Lakini
kutokana na upendu wa Mungu, alituongezea maarifa na vipaji mbalimbali
vilivyotuwezesha kutawala mazingira kwa manufaa yetu na viumbe vingine ndio
maana leo hii binadamu licha ya kutokuwa na maguvu kama walivyo wanyama wengine
Tembo na Simba tumeweza kujenga majumba kuishi kwenye mazingira mazuri na
yakliyo bora, kupata huduma za afya na elimu.” Alifafanua na kuongeza Tembo na
mahguvu yake, Simba na magubvu yake wao bado wako pori ni na hawajabadilika kwa
miaka yote hiyo.
Alitoa
mfano wa ndege aitwaye Tai (Eagle) ambaye ana nguvu nyingi, kucha kali zenye uwezo
wa kuchakura na kupokonya, mdomo wenye chongo kali na anakadiriwa kuishi hadi
miaka 50, lakini watafiti wengi wanase kabla ya kufikisha miaka hiyo 50 Tai ama
Eagle hufa kabla ya kufikisha umri huo kutokana na viungo vyake
vinavyomuwezesha kupata chakula, kutishiwa nguvu hizo, kwani nkucha hupinda na
hivyo hushindwa kupokonya na kuchakura vyakula, mdomo nao hupinda na hivyo
uwezo wake wa kudonoa nao hupungua na hatimaye hufa kwa sababu hawezi tena
kujitafutia chakula.
 “Hii
ndiyon tofauti ya wanyama wengine na binadamu kwani sisi tumejengewa maarifa
kwa hivyo tunatumia maarifa hayo kutatua kero mbalimbali na hivyo kishi kwa
furaha.” Alisema Padri Jiso.
Kwa
kutumia mfano huo Padri Jiso alisema ndio maana watoto hujengewa msingi
mzuri wa maarifa kwa kupatiwa elimu ili hatimaye baadaye waweze kutawala
mazingira wanayoishi kwa kuwa  wananachi
wazuri na wenye faida kwa taifa na jamii kwa ujumla.
Padri
huyo aliwaonya wanafunzi hao kuwa lazima watambue, adhabu walizokuwa wanapata
wakiwa shuleni ni adhabu za upendo zilizolenga kuwarekebisha ili kujaza maarifa
kwenye vichwa vyao kwa faida ya baadaye na kwamba nje ya mazingira ya shule
adhabu wataakazopata ni za “chuki” na hazina upendo wowote zaidi ya kuwuadhibi
ili kuleta majuto.
Katika
mahafali hayo pamoja na mabo mengine, wanafunzi walkikabidhiwa vyeti (Living
certificates)
na kushuhudia burudani mbalimbali zilizoporomoshwa na wanafunzi
wenzao.
Mtihani
wa taifa wa darasa la saba unatarajiwa kufanyika nchini kote kuanzia Septemba
11, 2019.
Mlulu Khalfan Said (kulia), akipokea cheti cha kuhitimu elimu ya
msingi (Darasa la VII) kutoka kwa Padri Jiso kutoka Mtakatifu Vincent wakati wa sherehe za
Mahafali ya Saba Shule ya Carmel Convent iliyoko Wilayani Mkuranga Mkoa wa
Pwani Agosti 31, 2019.