Home Mchanganyiko MKUTANO MKUU RSA WAFANYIKA JIJINI MWANZA 

MKUTANO MKUU RSA WAFANYIKA JIJINI MWANZA 

0

Muwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Marlin Komba,akizungumza na mabalozi katika mkutano mkuu uliofanyika Jijini Mwanza leo.30/8/2019.Picha zote na habari zimeandaliwa na Vero Ignatus
John Seka Afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama barabarani Nchini.(RSA )akizungumza na mabalozi katika mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika Jijini Mwanza.

 Naadhi ya mabalozi wa Usalama barabarani wakiwa katika picha ya pamoja kuelekea katika mkutano mkuu wa mwaka Jijini Mwanza leo 30/8/2019

 Mabalozi wa usalama barabarani wakionekana katika picha ya pamoja Jijini Mwanza leo tarehe 30/8/2019

Mwawakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Marlin Komba ,akisisitiza jambo katika mkutano mkuu wa mwaka wa mabalozi wa usalama barabarani uliofanyika Jijini Mwanza leo.30/8/2019

Mabalozi wa usalama barabarani nchini wakiwa katika mkutano mkuu wa Mwaka uliofanyika Jijini Mwanza leo 

 Moja ya timu wapenzi na madhafiki wa Simba sports Club wakiwa uwanjani kwaajili ya mchezo wa kirafiki katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.

Moja ya timu wapenzi na madhafiki wa Yanga  sports Club wakiwa uwanjani kwaajili ya mchezo wa kirafiki katika Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.

……………….

Na .Vero Ignatus ,Mwanza

Zaidi ya
mabalozi 125 kutoka Taasisi ya Mabalozi wa usalama barabarani( RSA )wamekutana  Jijini Mwanza,lengo kuu likiwa ni  kutoa Elimu na kuwajengea wananchi  uwezo wa  kuwa sehemu ya mabadiliko ya usalama
barabarani ikiwa ni namna  ya kusaidia
kupunguza ajali ,kwani kila raia wa Tanzania anawajibu wa kuwa sehemu ya
mabadiliko ya usalama barabarani.
 
John Seka Afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya
mabalozi wa usalama barabarani Nchini, amesema kwa kushirikiana na jeshi la Polisi
Kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Mwanza kikisimamiwa na RTO,Tanroad ,Jeshi
la zimamoto, walifanya zoezi za kurudishia alama za barabarani zile zilizopauka
,na kuchora mpya sehemu zinazohitajika.
 
Seka amesema kuwa kazi zao kubwa  kama RSA ni kukemea, kuelimisha ,kutoa taarifa
pale dereva anapokwenda kinyume na taratibu na sheria za usalama barabarani ili
kuhakikisha kuwa ajali zinapungua kama siyo kwisha kabisa
 
Sisi tunafanya kazi zetu kama polisi
jamii,macho yetu tunayaelekeza kwa kutambua kuwa jeshi la polisi peke yao
hawawezi kwani askari ni wachache na vitendea kazi ni vichache je! sisi kama
wananchi hatuna wajibu wa kupunguza?aliuliza Seka.”
 
Augustus Fungo ni Mkurugenzi wa tafiti za kisheria kutoka RSA amesema
kuwa pamoja na kuwa balozi lazima wazingatie sheria za usalama barabarani pia lazima
wafuate sheria kama utaratibu unavyoagiza
Amesema
hadi sasa RSA wanatekeleza mradi  wa Maboresho
ya sheria ya  usalama barabarani,wenye
lengo la kushawishi serikali na bunge kubadili sheria ya usalama barabarani ya
mwaka 1973  ili ikidhi mahitaji ya wakati
huu kwasababu ina mapungufu katika maeneo mbalimbali.
 
’’Mfano wa mapungufu hayo ni pamoja na
sheria ya sasa kutomlazimisha abiria kuvaa kofia ngumu,kufunga
mkanda,kutokulazimu magari madogo kuwa na vizuizi vya watoto wakiwa ndani ya
gari (child restraint) Sheria pia hailazimishi magari yote kusimama kabla ya
kuvuka kivuko cha reli isipokuwa magari ya abiria na mizigo .Alisema Fungo’’
 
Amesema
hadi sasa RSA imefanikiwa kufungua klabu za usalama barabarani kwa wanafunzi
katika shule 22,ambapo 10 kutoka mkoa wa Kilimanjaro,12 mkoa wa Pwani, amesema
matazamio ya baadae ni kupanua wigo wa shule zinazopata elimu ya usalama barabarani
nchini Tanzania.
 
“Kwa kuwa tunaamini watoto wakifundishwa
tangia wakiwa wadogo ni rahisi wao kuelewa zaidi kwao kutii sheria na
kujiepusha na ajali”alisema Fungo
 
Akizungumza
muwakilishi wa Katibu mkuu wizara ya mambo ya Ndani Marlin Komba amemtaka kila balozi kutimiza wajibu wake kwa
kuzingatia maadili,bila kuwa na ushabiki wowote,pasipo kuwatetea wavunja sheria
za usalama barabarani,badala yake watumie ubalozi wao kwenye kuelimika na kupata
maarifa.
 
“Kama wewe mwenyewe huwezi kuwa na
nidhamu mahali unapooneka je ukiwa peke yako utaionyesha ,nidhamu ni kusikiliza
na kuelewa
“alisema Marlin
 
Amewataka
kwenda kuwa mabalozi kwa watu wengine ili kufanya maamuzi sahihi kuzingatia
sheria na usalama barabarani ,nakuepuka lugha za matusi kwani ni kosa la
jinai,huku akiwaonya baadhi ya mabalozi kutokutumia nembo ya RSA kukashifu watu
wengine,amewataka kutumia utaratibu unaostahili
 
Siku
hiyo ya mabalozi wa usalama barabarani imebeba kauli mbiu isemayo ,uchumi wa
viwanda unahitaji kufanyika kwa mabadiliko ya sheria ya Usalama Barabarani,ili
kulinda rasilimali watu dhidi ya ajali.  Mkutano huo uliambatana na michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa mpira wa miguu,kuvuta kamba kufukuza kuku na mbio za magunia ,ambapo michezo yote ilifanyika katika uwanja wa mpira wa Nyamagana Jijini Mwanza.
aj28dec2014 ysajili 2015ali