Balozi wa Canada nchini, Pamela O’Donnel (kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ndogo ya Waziri Lugola, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Balozi wa Canada nchini, Pamela O’Donnell, masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Nchi ya Canada na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ndogo ya Waziri Lugola, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimkaribisha ofisini kwake, Balozi wa Canada nchini, Pamela O’Donnell. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika ofisi ndogo ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam, leo, walikubaliana kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Canada. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
**************
Na Felix Mwagara, MOHA.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini, Pamela O’Donnel na kumuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini.
Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Lugola, jijini Dar es Salaam, leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na ofisi ya Balozi huyo nchini.
Waziri Lugola alimuakikishia Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini.
“Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola.
Kwa upande wake Balozi Sara, alimshukuru Waziri Lugola kwa mazungumzo waliyoyafanya na kumuhakikishia ushirikiano zaidi kati ya Canada na Tanzania.