Home Mchanganyiko Taasisi ya family Federation for world peace yaahidi kumaliza upungufu wa damu...

Taasisi ya family Federation for world peace yaahidi kumaliza upungufu wa damu nchini

0

Baadhi ya wanachama wa federation wakichangia damu katika hospital ya taifa Muhimbili kitengo cha damu

Mratibu wa taasisi ya family Federation Bw. Semeni Kingaru

Muuguzi muhandamizi katika Hospital ya Muhimbili kitengo cha damu Judith Mayombo

*****************

Na Stahmil Mohamed

Taasisi ya family Federation for world peace yaahidi kumaliza upungufu wa damu nchini kwa kuendesha zoezi la uchangiaji damu kila mwisho wa wiki ili kuokoa watu mbalimbali wenye uhitaji wa damu.

Akizungumza kwa niaba ya kiongozi wa taifa wa shirikisho hilo wakati wa uchangiaji damu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili Bw Semeni Kingaru ambaye ni mratibu wa masuala mbalimbali ya taasisi hiyo amesema kuwa kutokana na uhaba wa damu uliopo nchini taasisi hiyo ambayo inawanachama zaidi ya  elfu 80 wameanzisha utaratibu wa uchangiaji damu kila mwisho wa juma lengo hasa ni kupunguza changamoto hiyo pia kuokoa maisha ya watu mbalimbali wenye uhitaji Wa damu wakiwemo majeruhi wa ajali, wanawake wajawazito wanaokwenda kujifungua hata watoto wenye uhitaji wa damu.

Kingaru ameendelea kwa kusema kuwa kutokana na hamasa waliyonayo wanachama Wa taasisi hiyo katika suala la uchangiaji damu wanaamini kuwa uhaba wa damu utapungua na watu mbalimbali wataweza kuokoa maisha kama ilivyo kauli mbiu yao ya ishi kwa ajili ya wengine .

Irene na Nasibu Mbarook  ni wanachama wa family Federation waliojitokeza katika kuchangia damu katika hospital ya Taifa ya Muhimbili wamesema kuwa wameamua kuchangia damu katika hospital hiyo Kwani wanajua uhaba wa damu uliopo katika hospital hiyo ya taifa Kwani kuna watu mbalimbali wenye uhitaji wakiwemo majeruhi wa ajali.

Kwaupande wake Judith Mtayombo Ambae ni muuguzi muhandamizi katika kitengo cha damu katika hospital ya muhimbili amewataka watanzania kujijengea utaratibu Wa kuchangia damu Kuwaokoa wagonjwa mbalimbali waliopo wodini pia inapotokea majanga makubwa kusiwepo na changamoto ya upatikanaji wa damu.