Home Mchanganyiko OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA WARSHA KUHUSU UTEKELEZEJI WA MARUFUKU YA...

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA WARSHA KUHUSU UTEKELEZEJI WA MARUFUKU YA MIFUKO YA PLASTIKI KWA MAAFISA MAZINGIRA WA MIKOA TANZANIA BARA

0

Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Kemilembe Mutasa akiongea na Wajumbe wa kikao kinachohusu Katazo la mifuko ya plastiki,  kilichoshirikisha Maafisa Mazingira wa Mikoa ya Tanzania kikao hiko kimeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma katika ukumbi wa Nyaraka.

Injinia Joseph Kiruki kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akitoa mada juu ya katazo la  mifuko ya plastiki katika kikao cha Maafisa Mazingira wa Mikoa kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kilichofanyika jijini Dodoma

Mwanasheria kutoka Baraza la Usimamizi wa hifadhi ya Mazingira (NEMC) Bwana Vincent Haule akifafanua jambo wakati wa kikao cha Maafisa ya Mazingira wa Mikoa kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma

Sehemu ya Wajumbe waliohudhsuria kikao cha Maafisa Mazingira wa Mikoa wakifuatilia mada kwa makini wakati wa kikao cha Maafisa Mazingira wa Mikoa kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.