Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario akiongoza ya misa takatifu ya Jubilei ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Salekio Kesyy iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Yohani Mtume ,Parokia ya Iwa-Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga .
MWENYEKITI
wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ambaye pia ni Mwenyekiti wa
taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amewapa neno wakuu wa
nchi 16 zinazounda Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), katika mkutano ujao kufikiria kuja
na ajenda ya pamoja ya sera moja ya elimu inayofanana.

Mbatia
amesema kuwa kama itakuwapo dhamira ya pamoja ya kuwa na sera hiyo ya
elimu kwa wanachama wa SADC, kunaweza kubadili sura ya Afrika na mageuzi
makubwa yakaonekana kwa miaka 20 yakisadifu mfumo wa elimu wa nchi za
Ulaya.

Mbatia ametoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa ibada ya misa takatifu ya Jubilee ya fedha
ya miaka 25 ya Padri Thomas Salekio Kessy, iliyofanyika katika Kanisa
la Mtakatifu Yohani Mtume, Parokia ya Iwa-Kirua Vunjo, mkoani
Kilimanjaro.

Ibada hiyo
iliongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Mhashamu Rogathe
Kimario, akisaidiwa na Msimamizi wa Jimbo Katoliki la Moshi na Wakili wa
Askofu, Deogratius Matiika.

“Kwa
mfano, majuzi nilisikia na kusoma baadhi ya maandiko kwamba watu wa
Namibia wao wanasema mfano mwanafunzi anayetoka Tanzania na amemaliza
kidato cha sita na akienda kwao, kupata Chuo Kikuu kule ni shida, kwa
sababu Namibia wao mfumo wao ni mgumu, wao elimu zao wanamalizia kidato
cha nne. Unajiuliza hivi silabasi zetu zimeundwa namna gani, nawashauri
wakuu wa nchi wanachama ni vizuri tukawa na sera moja ya SADC katika
masuala ya elimu,”alisema

Mwaka
huu, Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa SADC ikiwa imepita
miaka 16, tangu mkutano kama huo kufanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2003
chini ya utawala wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Kuhusu
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, kuweka mikakati ya
kuziwezesha nchi wanachama kufikia malengo ya kuelekea kwenye ukuaji wa
uchumi wa kati utakaokuwa maendeleo ya viwanda, Mbatia alisema:

“Mimi
nina ushauri kwa SADC, pamoja na mambo ya viwanda na mambo mengine yote
ambayo ni muhimu, wakuu wa nchi 16 wajitahidi sana kuhakikisha nguvu
kazi ya SADC ambayo ni vijana, wanapata elimu ambayo ni ujuzi na
wanaweza kuzalisha kwenye viwanda, wanaweza kuondoa masuala ya
umasikini, njaa, watu wakawa na afya njema lakini penda tusipende ni
lazima tuangalie je mifumo yetu ya elimu ikoje,”alieleza

Alisema
malengo hayo yanatekelezeka, lakini sharti nchi wanachama wawe
wamejiandaa vizuri na kwa utafiti alioufanya, bado kuna kazi kubwa mbele
ya safari, na akashauri zaidi kuwa malengo hayo yasiwe ya maneno,
yaende kwenye vitendo zaidi

. | ||