Watuhumiwa wa kesi ya uzururaji wakipanda katika gari
ya polisi kuelekea katika mahakama ya mwanzo ya Nunge, iliyopo
Manispaa ya Morogoro
***************
Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro limewafikisha mahakamani
watuhumiwa 30 kwa makosa ya uzembe na uzururaji hususani
katika kipindi cha usiku katika manispaa ya Morogoro.
Watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 16 mwaka huu katika eneo
la Kahumba Manispaa ya Morogoro,eneo ambalo maarufu kwa
biashara haramu za binaadamu huku baadhi ya wanaweke
hujihusisha na shughuli ya kuuza miili yao.
Watuhumiwa hao wakiwemo wanaweke 23 na wanaume 7
walikamatwa katika eneo hilo agosti 16 mwaka huu majira ya saa
6 usiku katika oparesheni iliyofanywa na jeshi la polisi wa doria
wakiongozwa na mkaguzi Copro Anold Njiro.
Aidha baada ya kufikashwa mahakamani watuhumiwa
wamesomewa mashitaka yanayowakabili na Hakimu wa
Mahakama ya mwanzo ya Nunge Emelia Mwambagi,ambapo
amesema kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa
mawili ambayo ni uzembe na uzurulaji pasipo sababu.
Hata hivyo watuhumiwa wote wamekana mashitaka hayo na kesi
hiyoitasomwa tene agosti 20 mwaka huu kutoka na kutokuwepo
kwa mashahidi kwa upande wa mashitaka huku baadhi ya
watuhumiwa wakiachiwa kwa dhamana ya kila mmoja kuwa na
mdhamini mmoja atakaye saini bondi ya shilingi milioni moja.