Home Mchanganyiko ASAS za kiraia zatakiwa kufanya kazi na serikali kuhudumia jamii

ASAS za kiraia zatakiwa kufanya kazi na serikali kuhudumia jamii

0

Washiriki wakiwa darasani kuendelea na mafunzo

Mkufunzi kutoka THRDC wakili Deo Bwire akitoa mafunzo kwa washiriki wa mafunzo kutoka asasi za kiraia mkoa wa Njombe na Iringa jana.

***************

NA  Francis Godwin,Iringa 

WITO  umetolewa  kwa mashirika ya utetezi  wa  haki  za  binadamu   nchini  kuendelea  kufanya  kazi ya  kuisaidia   serikali katika masuala  mbali mbali ya  kijamii  kama afya,elimu  na mengine ambayo  ambayo  serikali  imekuwa  ikifanya.
 

Akizungumza  wakati wa ufunguzi  wa mafunzo ya  siku  tatu  kwa washiriki wa mafunzo hayo kutoka asasi  za  kiraia  kanda ya nyanda  za  juu kutoka  mkoa wa  Njombe na Iringa  jana . mwezeshaji  wa mafunzo hayo  kutoka mtandao wa  watetezi wa  haki za  binadamu Tanzania (THRDC), wakili  Deogratias Bwire .

Kuwa  ipo  dhana  potofu  kwa  jamii juu ya  kazi  za  watetezi  wa haki  za  binadamu kwa  kumuona mtetezi kama  ni mchochezi   jambo  ambalo  si  sahihi  kwani   mtetezi  ni  mtu  yeyote anayefanya kazi  ya  kusaidia  kuokoa maisha  ya mwingine.

Alisema  kuwa mwaka   1998 baraza kuu la umoja  wa mataifa  lilidhia  azimio la haki za  binadamu japo  kwa  vipindi  tofauti  tofauti matamko  mbali mbali yalitolewa na hadi  nchi mbali mbali ziliweza kuja na  sera ya  haki ya  binadamu japo kwa Tanzania bado hatujawa na sheria  ama  sera ya  kuwatambua watetezi.

Kuwa matamko  ambayo yamepata kutolewa  kikanda ni kama  tamko la  Grad Bay la  mwaka 1999 ,tamko  la  Kigali la  mwaka 2003 ,makubaliano  2004 (Mwakilishi wa  watetezi ) , mpango wa kikazi wa Kampala ( KAPA 2009)  huku  kitaifa  ni THRDC (makubaliano ya  Newafrica Hotel).

“Nani  mwenye jukumu kumlinda  mtetezi  ,azimio  la watetezi wa Haki za  binadamu linasisitiza  kwamba  nchi  ndiyo  ya kwanza  katika kuwalinda  watetezi  wa Haki za binadamu “  alihoji  Bwire.

Aidha  alisema kuwa makundi na miungano inayochangia katika  kuboresha ukiukaji wa  haki  za binadamu na uhuru wa  kimsingi  hivyo basi ukiangalia  ibara  ya 12  ya  tamko hiloinatamka  wazi  kwamba dola ina mamlaka ya  kumlinda mtetezi wa haki za  binadamu .

Alizitaja  haki  za mtetezi  kuwa ni  kulinda  na  kustawisha haki  za  binadamu ,kulindwa , kuchunguza na kupata  habari  ,kutoa maoni ,kukusanyika kwa amani ,kuunda  asasi  na kupata fedha  za  miradi  pamoja na kuweza kuifikia mahakama.

Bwire  alisema kuwa  watetezi wa haki za binadamu  wanatambulika  kote duniani  na  serikali  inajukumu la kuwalinda  watetezi  ,lakini sote tuna jukumu hilo na  THRDC ni  mtandao  kwa  ajili ya watetezi .

Hivyo  alisema  kuwa  mafunzo ya utetezi wa Kimkakati na usalama kwa Watetezi wanaofanya kazi za utetezi wa haki za Kijamii kwa mikoa ya Iringa na Njombe  ambayo yameandaliwa na THRDC ni kuweza  kuwajengea  uwezo  zaidi ili kuifanya kazi  hiyo kwa ufanisi .

“Haki za Kijamii zitakazofundishwa zinahusisha haki  za elimu bora, afya bora, chakula, maji safi, malazi yenye staha na haki za hifadhi ya jamii (social security) pamoja na mambo mengine” alisema .

 Alisema  watetezi hao watajengewa uwezo juu ya mabadiliko ya 2019 ya sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikari ya mwaka 2002 na kuelekezwa namna bora ya kufuata sheria za Mashirika yasiyo ya kiserikali na sheria nyingine za nchi kama njia mojawapo ya kuhakikisha usalama wa Mashirika hayo.

Wakitoa  maoni yao  katika mafunzon hayo washiriki wa mafunzo hayo  walisema kuwa  wengi  wao  wamekuwa  wakifanya kazi ya  utetezi  bila  kujua   wao  wanafanya kazi  ngani na  wakati  mwingine wanakuwa  katika mazingira  magumu  pasipo  kujua  nani  wa  kumtetea .
Kuwa  aliwataka  watetezi hao  kutoogopa  sheria  zilizotungwa  badala yake  kufanya kazi zao kwa  uhuru  zaidi  huku  wakitambua  sheria  na mazingira ya  kazi ya  utetezi .

Hivyo  kupitia mafunzo hayo ni wazi  wanaweza kupiga hatua ya kuboresha  kazi zao na hata  kuisaidia jamii na serikali katika  uwajibikaji wake  wa  kila  siku  wenye lengo la  kusaidiana pamoja   kuhudumia  jamii.