Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, akiwataka watumishi wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, kufanya kazi kwa weledi, alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam, kubaini changamoto za utekelezaji wa bajeti yake ya mwaka 2018/19 na njia za kuzitatua.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kulia), akiwa na mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, Dkt. Geraldine Rasheli (kushoto), alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, Dkt. Geraldine Rasheli, akieleza changamoto za utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/19, hususani kwenye miundombinu ya kuhifadhi mafuta, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), katika ofisi za taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Christopher Nkupama (kulia) na Mtaalam wa Sera wa Wizara hiyo Bw. Msabaha Msabaha, wakifuatilia kwa makini maelezo ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, Dkt. Geraldine Rasheli, wakati wa ziara ya kufuatilia changamoto za utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/19 kwa taasisi hiyo na njia za kuzitatua.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, wakifuatilia kwa makini Mkutano kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, Dkt. Geraldine(hawapo pichani), katika Ofisi za GPSA, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masuala ya Biashara wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, Bw. Malik Aram (kulia), akieleza changamoto ya visima vya mafuta, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu ya kufuatilia changamoto za utekelezaji wa Bajeti ya taasisi hiyo kwa mwaka 2018/19.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)
*************
Serikali inaangalia njia mbadala ya ununuzi wa magari yake kwa kwenda moja kwa
moja kiwandani bila kupitia kwa mawakala kutokana na gharama kuwa juu na
hazitabiliki.
Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt.
Khatibu Kazungu, alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala wa Huduma ya
Ununuzi Serikalini (GPSA), jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubaini changamoto na
mafanikio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/19 kwa taasisi hiyo.
Dkt. Kazungu alisema kuwa, ununuzi wa magari ya Serikali unatumia gharama kubwa
kutokana na kuwatumia Mawakala wa Ununuzi ambao bei zao ni za juu na zinabadilika
mara kwa mara, hivyo kuna haja ya kwenda moja kwa moja kiwandani ili kuokoa fedha
za walipakodi zinazopotea.
Aidha Serikali inaangalia namna itakavyo boresha miundombinu ya GPSA hasa kwa
kuwekeza katika Visima vya mafuta ili kuwa na mafuta ya kutosha hivyo kusaidia
kuongeza ufanisi katika kuhudumia magari ya Serikali.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa GPSA, Dkt. Geraldine Rasheli, alimshukuru
Dkt. Kazungu, kwa kutembelea taasisi yake na kuahidi kuyafanyia kazi maagizo
yaliyotolewa ili kupunguza malalamiko katika utoaji huduma na kuongeza tija kwa Taifa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Kazungu, anaendelea na
ziara ya kikazi katika taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, kuangalia changamoto za
utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/19 na njia za kuzitatua kwa bajeti ya mwaka
2019/20.