Wananchi wakipata huduma za usajili laini za simu kwa alama za vidole pamoja na usajili wa kupata kitambulisho cha Taifa cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Afisa akiwahudumia wananchi katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kusini
Wananchi wa Lindi na viunga vyake wakipata huduma za usajili laini za simu kwa alama za vidole katika banda la TCRA ambapo NIDA na watoa huduma walikuwepo.
*************
Na mwandishi Wetu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) imesema kuwa wananchi wa Kanda ya Kusini watumie maonesho ya Nane Nane kupata elimu ya Mawasiliano pamoja na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.
Hayo ameyasema Afisa wa TCRA Abdulrahaman Millas katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kusini mkoani Lindi , amesema maonesho ya Nane Nane yatumike kwa wananchi kusajili laini za simu alama za vidole kwa huduma zote za kufanya usajili zipo ndani za maonesho hayo.
Millas amesema muda uliokuwepo wananchi kusajili laini za simu kwa alma za vidole kwani mwisho wa usajili huo ni Desemba 31 mwaka huu.
Amesema kuwa muda uliopangwa lazima utumike kikamilifu kupunguza kujazana kwa watoa huduma katika tarehe za mwisho za Desemba.
“Muda umewekea ni mkubwa kwa wananchi kupata kitambulisho cha Taifa na kusajili laini zao za simu na walio na vitambulisho vya Taifa kusajili laini zao za simu kuondokana na usumbufu wa kufungiwa mawasiliano simu hizo.
Aidha amesema kuwa TCRA iko bega kwa bega katika kutoa elimu kwa wananchi kwa huduma mbalimbali za mawasiliano ili wasitumie mawasiliano kinyume cha sheria.