*************
-Na Kaka mkuu MaCsmillan Akyoo II
Baada ya Frank lampard kuwasili Chelsea kama kocha mkuu wengi wamekuwa na maswali yasiyo na majibu kuhusu idadi kubwa ya viungo waliopo Chelsea.
Kwenye eneo la ukabaji kuna viungo bora kama Ngolo Kante na Jorginho Frellò hawa wote ni viungo professional in nature kwenye eneo la Difensive Midfielder, Kante ni bora kwenye difensive role na kwenye tackles and blocks, Joginho ni bora kwenye kupooza mashambulizi, kubalance timu kwenye eneo la nyuma na kutuliza pressure, hapa itategemea Lampard atatumia mfumo gani ili mmoja wao aingie kwenye first11 yake.
Kwenye eneo la Centre midfielder kuna viungo bora kama Loftus Cheek na Tiemoue Bakayoko, Loftus ni bora zaidi kwenye attacking role, kumiliki mpira na kutengeneza nafasi hasa kwenye eneo la kati, Bakayoko ni bora zaidi kwenye earial duel na difensive role japo kwenye eneo hilo ana madhaifu madogo madogo ya wapi apeleke mpira na kwa wakati gani.
Kwenye attacking role kuna Mateo Còvasic na Ross Barkley, Còvasis ni bora kwenye kumiliki mpira, kutengeneza nafasi na kutengeneza pass za magoli,
Barkley ni kiungo mzuri kwenye kufunga na kuasist.
Hawa wote wanafaa kuanza kwenye First Eleven ya Chelsea japo itategemea Lampard atakuja na mifumo gani kwenye ligi kuu ya Epl.
All the Best Frank Lampard