Home Mchanganyiko MBUNGE DITOPILE AMSHUKURU RAIS DKT.MAGUFULI UZINDUZI WA MRADI WA UMEME WA...

MBUNGE DITOPILE AMSHUKURU RAIS DKT.MAGUFULI UZINDUZI WA MRADI WA UMEME WA MTO RUFIJI

0

Mbunge wa vijana Taifa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Nishati na Madini Mh Mariam Ditopile kwa niaba ya vijana amemshukuru Rais Magufuli kwa uzinduzi wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji Mkoani Pwani kupitia bwawa la kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki na kati, utakaogharimu kiasi cha Shilingi Trilioni 6.5.

Mradi huo unategemewa kukamilika mwezi June 2022 utazalisha megawati 2115 na unatajwa kuwa mwarobaini wa umeme jambo ambao litachochea ukuaji wa Tanzania ya viwanda.

” Nina imani sasa ile ahadi ya Tanzania ya viwanda kupitia chanzo hiki cha uhakika na cha gharama nafuu cha Umeme inaenda kutimia rasmi sanjari na uhakika wa umeme wa kutosha ktk mradi mkubwa wa treni ya mwendo kasi (SGR).

Sisi kama vijana hatuna budi kuishukuru serikali yetu sikivu chini ya Rais wetu kipenzi Dk Magufuli na wasaidizi wake wote kwa kuisimamia vyema na kwa dhati kabisa miradi hii, kwani vijana ndio tunaenda kuwa wanufaika wakubwa,” amesema Mhe Ditopile.

Amesema kupitia miradi hii kuna ajira za kudumu na ajira za vipindi maalum zitazaliwa jambo ambalo litapunguza wimbi kubwa la vijana ambao hawana ajira.

” Kupitia miradi hii kuna fursa mbalimbali za kibiashara kwa mfano, mahoteli, migahawa, mama lishe, vifaa mbalimbali vya ujenzi.

Pia itakapokamilika miradi hii kwa upande wa wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla tutakuwa na umeme wa uhakika na kushuhudia ndoto ya Rais Magufuli kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati kupitia viwanda.

Mhe Ditopile amesema kwa upande wa wakulima kupitia treni ya umeme utakaotokana na mradi huo wa Stiglera Gorge watakuwa na uhakika wa kupata soko lenye tija.

” Kwenye hili tunamuahidi kwa dhati kabisa Rais wetu tupo nae bega kwa bega kwa kuwa Watanzania wa leo wanataka kazi na serikali yetu chini ya Rais Magufuli sasa ipo kazini,” amesema Mhe Ditopile.