Home Mchanganyiko TUMEAMUA KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA YA KUWATAMBUA WAKULIMA WOTE NCHINI-MHE HASUNGA

TUMEAMUA KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA YA KUWATAMBUA WAKULIMA WOTE NCHINI-MHE HASUNGA

0

Sehemu ya Wakazi wa kijiji na kata ya Kilimampimbi wakimlaki mbunge la Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo wakati alipowasili kijijini hapo tarehe 25 Julai 2019 akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo jimboni humo. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Sehemu ya Wakazi wa kijiji na kata ya Kilimampimbi wakimsikiliza mbunge la Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo wakati akihutubia wananchi kijijini hapo tarehe 25 Julai 2019 akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo jimboni humo.

Wakazi wa kijiji cha Ikomela kilichopo kata ya Kilimampimbi wakimsikiliza mbunge la Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo wakati akihutubia wananchi kijijini hapo tarehe 25 Julai 2019 akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo jimboni humo.

Wananchi wa kijiji cha Chizumbi kilichopo kata ya Isandula wakimsikiliza mbunge la Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo wakati akihutubia wananchi kijijini hapo tarehe 25 Julai 2019 akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo jimboni humo.

 

Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Wizara ya Kilimo inaendelea na mkakati madhubuti wa
kuwatambua wakulima wote nchini ili kuwa na ufahamu wa watu wanaopaswa kuhudumiwa
kwa ajili ya pembejeo za kilimo.

Mkakati huo wa wizara wa kuwatambua wakulima nchini
unahusisha usajili wa wakulima ili kubaini mahali wanapoishi, ukubwa wa
mashamba yao na mazo wanayolima.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 25 Julai 2019 na
Mbunge la Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa
Kilimo wakati akizungumza kwenye mikutano ya hadhara katika kijiji cha
Chizumbi, Ukwile, Chimbuya katika kata ya Isandula pamoja na Kijiji cha
Ikomela, Isandula na Kilimampimbi vilivyopo kata ya Kilimampimbi wakati wa
ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo jimboni humo.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya waTanzania
wanawategemea wakulima katika kukamilisha mahitaji yao lakini wakulima hao
hawatambuliki, hivyo mkakati wa utambuzi wa wakulima utaimarisha uwezekano wa
kuwahudumia ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Mhe Hasunga pia amewaeleza wananchi hao lengo la
serikali kuanzisha mradi mkubwa wa ujenzi wa treni ya kisasa itakayorahisisha
huduma za kijamii ikiwemo usafirishaji wa mizigo yakiwemo mazao ya wakulima.

Pia amesema kuwa serikali inaendelea na mchakato wa
kuwafikishia wananchi huduma bora ikiwemo upatikanaji wa umeme katika maeneo
yote vijijini.

Kuhusu sekta ya Kilimo Mhe Hasunga amesema kuwa
katika kipindi cha muda mrefu wakulima wamekuwa wakilima lakini matokeo yake
wanapata hasara au kipato cha kujikimu hivyo ili kupata faida na tija ni wazi
kuwa wakulima lazima wabadilishe mtazamo ili waweze kuwa na Kilimo chenye tija
na kibiashara.

Alisema wizara yake imejipanga kutoa elimu bora kwa
wakulima juu ya Kilimo ili kufuata taratibu za Kilimo bora zinazotolewa na
wataalamu mbalimbali wa Kilimo katika vijiji.

Kadhalika Mhe Hasunga amesikitishwa na wananchi
kutokula vizuri ilihali wao ndio wazalishaji wakubwa wa mazao ya mbogamboga na
matunda.

“Ukienda mahospitalini watu wengi wanaoumwa ni
wakulima, kwahiyo nawasihi wakulima mkizalisha chakula muwe wa kwanza kula
vizuri halafu ziada ndio mkauze” Alisisitiza Mhe Hasunga