Home Mchanganyiko USHIRIKI WA TAEC KWENYE MAONESHO YA NANE NANE MWAKA 2019

USHIRIKI WA TAEC KWENYE MAONESHO YA NANE NANE MWAKA 2019

0

****************

Arusha, Julai 25, 2019

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), inatarajia kushiriki kwenye
maadhimisho ya sherehe za kitaifa za Nane Nane kanda ya ziwa mashariki
yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu kuanzia tarehe
28 Julai hadi 10 mwezi Agosti, 2019.

Katika maadhimisho hayo, TAEC itaweza kuonesha shughuli mbali mbali
zinazofanyika katika Tume ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi na wadau
mbali mbali juu ya udhibiti na matumizi salama ya mionzi hapa nchini.

Elimu kwa wananchi juu ya matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwenye
sekta za afya, kilimo, viwanda, mifugo, maji, lishe pamoja na ujenzi inatolewa.
Wananchi wote wanakaribishwa ili kuweza kujipatia elimu bure kwa njia za
maelezo, video fupi, vipeperushi na majarida ili kujiongezea uelewa juu ya
majukumu yanayotekelezwa kisheria na TAEC katika Nyanja za udhibiti wa
mionzi na uhamasishaji wa matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia.