WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akiwa na
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu (kulia), wakiwasaka watumia
dawa za kulevya (mateja) ambao wanafanya matukio ya uhalifu katika
Bonde la Jangwani, Ilala, Jijini Dar es Salaam. Lugola alimpa saa nne
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, kuwakamata wahalifu hao na ifikapo
muda huo atafika kituo cha Polisi Msimbazi kwa ajili ya kuwaona
watuhumiwa hao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, ACP Zuberi Chembera, alipompigia simu
afike katika eneo la Bonde la Msimbazi, kuongeza kasi ya kuwasaka
watumia dawa za kulevya (mateja) ambao wanatuhumiwa kufanya matukio
ya ukabaji, na upora wa mali za watu mbalimbali katika eneo hilo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kulia) akiwa na
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan Zungu (wapili kulia), wakiwasaka
watumia dawa za kulevya (mateja) ambao wanafanya matukio ya uhalifu
katika Bonde la Jangwani, Ilala, Jijini Dar es Salaam. Lugola alimpa saa nne
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, kuwakamata wahalifu hao na ifikapo
muda huo atafika kituo cha Polisi Msimbazi kwa ajili ya kuwaona
watuhumiwa hao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
*************
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefanya operesheni
ya kuwasaka na kuwakamata mateja mbalimbali ambao wanatumia dawa
za kulenya na kufanya uhalifu katika bonde la Jangwani, Ilala, jijini Dar es
Salaam.
Lugola ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azan
Zungu, kuwasaka mateja hao ambao wanatumia aina mbalimbali ya
madawa ya kulenya, baada ya kuona viongozi hao wanawasaka walikimbia
katika maeneo ya vijiwe vyao.
Waziri Lugola wakati akiwa katika operesheni hiyo ambayo ilidumu kwa saa
moja na nusu kwa kutembelea mitaa mbalimbali ya bonde hilo, alimpigia
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala-RPC, ACP Zuberi Chembera,
kufika katika eneo hilo huku akiwa na askari kwa ajili ya kuendeleza zoezi
hilo.
Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo ya Jangwani, leo, Waziri Lugola
alisema wahalifu hawa wanapaswa kusakwa kwa nguvu zote na
kukamatwa, kwasababu walishampora mtu katika mitaa hiyo na kumuaa.
“RPC kuanzia muda huu, nakuagiza askari wako waingie mitaani,
kuwakamata wahalifu hawa, na nitakuja saa 12 jioni ya leo, kuona wahalifu
wote katika bonde hili wamejaa katika kituo cha Msimbazi, na
muwakamate wahalifu na sio kuwaonea watu wasiokuwa na makossa,”
alisema Lugola.
Lugola aliongeza kuwa, Serikali haiwezi kukaa kimya kufumbia macho
matukio ya kiuhalifu ambayo yamekithiri katika eneo hilo na kuwafanya
wananchi kutopata usingizi kuhofia kuvamiwa kwa muda wowote usiku au
mchana.
Alimtaka Kamanda wa Polisi Mkoa huo, kuendelea kufanya operesheni ya
mara kwa mara kuwasaka wahalifu hao ambao wengi wao ni mateja
ambao wanatumia dawa za kulevya.
Kwa upande wake Mbunge Zunge, ambaye ndio alimwita Waziri huyo
kutembelea eneo hilo kuona kero kubwa awanazopata wananchi wake,
alisema wahalifu hao hawatoki pekee katika Jimbo lake, bali wengi wao
wanatoka maeneo mbalimbali katika Jiji la Dar es Salaam.
“Wenyeji wa eneo hili ni wachache, wengi wanatoka mitaa mbalimbali ya
hapa Dar es Salaam ikiwemo Temeke na kwingineko, hivyo mheshimiwa
Waziri tunajua utendaji wako, tunakuomba hii kero inatuumiza sana,
wananchi wanakosa amani kutokana na uwepo mkubwa wa wahalifu
hawa,’ alisema Zungu.
Waziri Lugola alisema Dkt John Magufuli anawataka wananchi wake waishi
kwa amani na utulifu, yeye Waziri hatakubali kuona matukio hayo ya baibu
yakishika kasi mitaani. Aliwataka Makamanda wa Polisi nchini kuwasaka
wahalifu muda wowote si mpaka yeye atoe agizo au atembeleee.