Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akiwafafanulia jambo,
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (kushoto) na
Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali
Charles Mbuge (kulia) wakati Waziri huyo alipokua anakagua ujenzi wa
nyumba zaa askari Magereza, zinazojengwa na JKT, Ukonga, jijini Dar es
Salaam. Lugola ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa
nyumba hizo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali
Charles Mbuge (kulia), akimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola (katikati), jinsi ujenzi wa nyumba za askari Magereza
ukiendelea, Ukonga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Lugola ameridhishwa na kasi ya
utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob
Kingu (wapili kushoto), akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Kangi Lugola (kushoto), wakati viongozi hao walipofanya ziara
Ukonga kuangalia ujenzi wa nyumba za askari Magereza ulipofikia. Lugola
ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo.
Watatu kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Phaustine Kasike, na
kulia ni Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia
Jenerali Charles Mbuge. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya nyumba za askari Magereza zinazojengwa na Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT), Ukonga jijini Dar es Salaam. Ujenzi huo umefikia asilimia 70.
Na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni. Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Kangi Lugola amefanya ziara katika eno hilo akiwa na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, wote wameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa
ujenzi wa nyumba hizo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, (kushoto) akimsalimia
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, wakati Waziri
huyo alipokua anawasili katika mradi wa ujenzi wa nyumba za askari
magereza, Ukonga, jijini Dar es Salaam, leo. Lugola ameridhishwa na kasi
ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
************
Na Felix Mwagara, MOHA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema ameridhishwa
na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za askari magereza
unaofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Ukonga jijini Dar es Salaam.
Waziri Lugola amesema Jeshi hilo linastahili pongezi kutokana na kasi ya
ujenzi wa nyumba hizo ambao umefikia asilimia 70 kukamilika.
Akizungumza mara baada ya kumaliza ukaguzi wa ujenzi huo, Lugola
amesema, atazungumza na Rais John Magufuli ili aweze kutoa kiasi cha
fedha kilichobaki kwa ajili ya kukamilisha asilimia thelathini zilizobaki ili
mradi huo ukamilike.
Lugola amesema, Jeshi la Kujenga Taifa lilikabidhiwa mradi huo zaidi ya
miezi miwili iliyopita kutoka kwa Wakala wa Majengo (TBA) kufuatia agizo
Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuonekana kusuasua kwake.
Waziri Lugola amesema, amefurahia kuona ujenzi huo ukiendelea vema na
kwa kasi kubwa na kuwapongeza askari hao kwa kazi kubwa wanayoifanya
na kusisitiza kuwa anataka kuona zaidi kauli ya Mkuu wa Ujenzi huo
akisema Jeshi halishindwi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob
Kingu, alisema amefurahishwa na kasi hiyo, na ana uhakika JKT ipo vizuri
na matumaini yake makubwa ujenzi huo utakamilika hivi karibuni.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Phaustine Kasike, amesema
kukamilika kwa ujenzi huo kutawezesha jumla ya familia 172 za askari
Magereza kuishi eneo katika makazi hayo huku ujenzi huo ukikadiriwa
mpaka sasa kutumia zaidi ya shilingi bilioni.