Home Mchanganyiko WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA NJOMBE

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA NJOMBE

0

**************

NJOMBE

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amezindua utoaji wa huduma za afya katika hospitali mpya ya rufaa ya mkoa wa Njombe iliyozinduliwa april 10 mwaka huu na rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dr Magufuli baada ya kuridhishwa na ubora katika ujenzi wake.

Uzinduzi huo umefanyika mara baada ya rais akiwa mkoani Njombe april 10 mwaka huu kuridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa awamu ya kwanza wa hospitali hiyo uliohusisha ujenzi wa wodi za wagonjwa wa nje OPD ambapo aliagiza hospitali hiyo kuanza mara moja kutoa huduma kwa wagonjwa huku ikishuhudiwa wagonjwa 20 wakitibiwa bure kuashiria kuanza kwa huduma.

Akifafanua mpango wa serikali katika kuboresha huduma katika hospitali hiyo ya rufaa waziri Ummy amesema serikali imepanga kupeleka madaktari bingwa wafani 13 pamoja na vifaa vya kisasa ili koboresha huduma katika hospitali hiyo huku akidai katika kufanikisha hilo tayari imetoa bil 2.2 za dawa na vifaa tiba ili kuwepo na ufanisi katika utoaji wa huduma .

Mbali na kuboresha matibabu waziri huyo pia amesema serikali imetoa bil bil 7.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa awamu ya tatu ya ujenzi wa hospitali hiyo ambao utahusisha ujenzi majengo saba zikiwemo , jengo la wazazi la ghorofa tatu, maabara , jengo la wagonjwa mahututi na upasuaji,jengo la wagonjwa ghorofa tatu na nyumba tano za watumishi zoezi ambalo limeenda sambasamba na kumkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi wa majengo hayo utakaofanyika kwa miezi nane.

Awali akizungumza mkuu wa mkoa wa Njombe Christophee Olesendeka amesema ili wagonjwa wafurahie huduma anamtaka mkurugenzi na mkuu wa wilaya kukutana wasafirishaji ili mabasi yafike hospitalini hapo huku mwenyekiti wa halmashauri Edwin Mwanzinga akiomba serikali kuto itupa iliyokuwa hospitali ya rufaa kibena

Baada ya maombi hayo Waziri Ummy Mwalimu anatoa agizo la kutohamishwa kifaa chochote katika hospitali hiyo huku pia akitaka bajeti iliyokuwa ikitumika kwa huduma za rufaa kubakishwa hospitalini hapo jambo ambalo linapokelewa vyema na wananchi.

Lakini wananchi wana maoni gani kuhusu kuanzishwa kwa utoaji wa huduma za afya katika hospitali ya rufaa ambao wanasema huduma za uhakika zimekuja nyumbani

Waziri Ummy amezindua huduma za afya na kukabidhi iliyokuwa hospitali ya rufaa kibena kwa halmashauri ya mji wa Njombe .