Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo Barbara Kambogi akizungumza na Raisi wa Shirikisho la Wasanii Simon Mwakifamba katika hafla ya usiku wa Jukwaa la kuwa na Staa na Maisha Magic Bongo iliyofanyika Hyatt Regency Hotel hivi karibuni. Katika hafla hiyo, Maisha Magic Bongo ilizindua awamu ya 3 ya tamthilia
ya Kapuni, Msimu wa 4 wa Harusi Yetu na kipindi kipya cha Mizani ya Ushambenga.
ya Kapuni, Msimu wa 4 wa Harusi Yetu na kipindi kipya cha Mizani ya Ushambenga.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda (katikati) akiwa na Katibu Mkuu wizara ya Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Suzan Mlawi (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa COSOTA Doreen Sinare (Kushoto) wakiwa katika hafla
ya usiku wa Jukwaa la kuwa Staa na Maisha Magic Bongo iliyofanyika Hyatt Regency Hotel hivi karibuni. Katika hafla hiyo, Maisha Magic Bongo ilizindua awamu ya 3 ya tamthilia ya Kapuni, Msimu wa 4 wa Harusi Yetu na kipindi kipya cha Mizani ya Ushambenga.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania Godfrey Mngereza akizungumza na Katibu wa Shirikisho la Sanaa Mathew Bicco wakati wa hafla ya usiku wa Julwaa la kuwa Staa na Maisha Magic Bongo iliyofanyika Hyatt Regency Hotel hivi karibuni. Katika hafla hiyo, Maisha Magic Bongo ilizindua awamu ya 3 ya tamthilia ya
Kapuni, Msimu wa 4 wa Harusi Yetu na kipindi kipya cha Mizani ya Ushambenga.
Kapuni, Msimu wa 4 wa Harusi Yetu na kipindi kipya cha Mizani ya Ushambenga.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania na moja ya muigizaji mpya wa tamthilia ya HUBA Piere maarufu kama “Piere Likwidi” wakati wa hafla ya usiku wa Jukwaa la kuwa Staa na Maisha Magic Bongo iliyofanyika Hyatt Regency Hotel hivi karibuni. Katika hafla hiyo, Maisha Magic Bongo ilizindua awamu ya 3 ya tamthilia ya Kapuni, Msimu wa 4 wa Harusi Yetu na kipindi kipya cha Mizani ya Ushambenga.
………………………….
Tamthilia ya Kapuni yaingia msimu wa 3
Msimu wa 4 wa Harusi Yetu nao kutikisa
Kipindi kipya cha Mizani ya Ushambenga kuanza
kurindima!
Tamthilia ya Kapuni yaingia msimu wa 3
Msimu wa 4 wa Harusi Yetu nao kutikisa
Kipindi kipya cha Mizani ya Ushambenga kuanza
kurindima!
Baada ya kiu ya muda mrefu, sasa wateja wa DStv kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo wataanza tena kushuhudia msimu mpya wa ile tamthilia yao pendwa ya Kapuni waliyokuwa wakiingojea kwa hamu, sambamba na msimu wa nne wa kipindi cha Harusi
Yetu bila kusahau kipindi kipya cha jarida kinachofahamika kama Mizani ya Ushambenga chini ya mtangazaji mashuhuri Mariam wa Migomba.
Yetu bila kusahau kipindi kipya cha jarida kinachofahamika kama Mizani ya Ushambenga chini ya mtangazaji mashuhuri Mariam wa Migomba.
Akizungumza wakati wa kusherekea usiku wa Jukwaa la kuwa Staa iliyofanyika jijini dar es Salaam hivi karibuni, Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo Barbara Kambogi alisema kuwa, “Nina furaha kubwa moyoni, kama Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo kushuhudia uzinduzi wa tamthilia ya Kapuni msimu wa 3, Harusi Yetu msimu wa 4 na kipindi kipya cha jarida, Mizani ya Ushambenga, kwa sababu wote waliohusika kuandaa vipindi hivi ambao ni wasanii pamoja na crew wamefanya kazi usiku na mchana kwa bidii mno.
Toka kuzinduliwa kwake October 2015, chaneli hii imekuwa mstari wa mbele kuonyesha kazi za wasanii wa Tanzania hapa kwetu nyumbani na pia nje ya mipaka yetu. Hivyo basi, tumeweza kupanua wigo wa kazi za wasanii hawa kuonekana kwenye
jukwaa la kimataifa na kuleta sifa kubwa nchini kwetu.
jukwaa la kimataifa na kuleta sifa kubwa nchini kwetu.
Ndani ya miaka minne, tumeweza kufanya vitu vingi kusaidia kuinua tasnia ya filamu Tanzania. Pamoja na kufanya ununuzi wa vipindi mbali mbali, pia tumeweza kufadhili vipindi tukishirikiana na watayarishaji kutoka hapa Tanzania. Kwa kufanya hivi, wasanii
wetu wameweza kujipatia ajira na kipato ili kuwawezesha katika maisha yao ya kila siku. Nadhani wengi wenu mnafahamu na kuvifuatilia vipindi hivi ambavyo ni Harusi Yetu, HUBA pamoja na Mwantumu.
wetu wameweza kujipatia ajira na kipato ili kuwawezesha katika maisha yao ya kila siku. Nadhani wengi wenu mnafahamu na kuvifuatilia vipindi hivi ambavyo ni Harusi Yetu, HUBA pamoja na Mwantumu.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso aliongeza kuwa , “Kwa hakika chanel hii imechangia sana katika kuimarisha tasnia ya sanaa hapa nchini hususan filamu na muziki. Hili ni swala jema kwani sote tulitamani sana sanaa yetu
igeuke kuwa kiwanda kikubwa cha kutoa ajira kwa vijana wetu na pia kuiletea jamii yetu na taifa zima kwa ujumla manufaa makubwa ya kiuchumi.
igeuke kuwa kiwanda kikubwa cha kutoa ajira kwa vijana wetu na pia kuiletea jamii yetu na taifa zima kwa ujumla manufaa makubwa ya kiuchumi.
Hili linathibitika wazi kwa uzinduzi huu uliofanyika usiku wa leo ambapo mbali na tamthilia pendwa ya Kapuni, Harusi Yetu na kipindi kipya cha Mizani ya Ushambenga ambayo mpaka kukamilika kwake zimehusisha takribani wasanii Zaidi ya 100 ambao ni
watanzania mbali na wafanyakazi wasaidizi mbalimbali kama mafundi, madereva na kadhalika kuweza kujipatia kipato.
watanzania mbali na wafanyakazi wasaidizi mbalimbali kama mafundi, madereva na kadhalika kuweza kujipatia kipato.
Sambamba na jitihada hizi zinazofanyika na chaneli ya Maisha Magic Bongo, kampuni ya MultiChoice pia imekuwa mstari wa mbele katika kuchochea ubunifu wa vijana katika tasnia ya filamu hapa nyumbani na Afrika kwa ujumla. MultiChoice imeanzisha academy maalum ya mafunzo ya filamu ijulikanayo kama MultiChoice Talent Factory Academy.Hii hutoa mafunzo ya mwaka mzima kwa vijana wetu wenye vipaji katika tasnia ya
filamu. Akademy hii inahusisha vijana kutoka kote barani Afrika na ina lengo la kukuza
vipaji na kuimarisha sekta ya filamu kote barani Afrika. Hivi sasa watanzania wane (4) wako kwenye akademi hiyo iliyopo nchini Kenya, alisema Jacqueline.