Home Mchanganyiko KANISA LA EFATAH LATAKIWA KUANDAA MPANGO KAZI WA KUENDELEZA NG’OMBE WA MAZIWA

KANISA LA EFATAH LATAKIWA KUANDAA MPANGO KAZI WA KUENDELEZA NG’OMBE WA MAZIWA

0

Akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa shamba la g’ombe wa Maziwa la Malonje leo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega ameitaka taasisi ya kidini ya Kanisa la EFATAH iliyopatiwa shamba la ng’ombe wa maziwa la Malonje baada ya kubinafsishwa na serikali mwaka 2007,kuandaa mpango kazi utakaosaidia kuendeleza ng’ombe wa mziwa na uzalishaji wa maziwa wenye tija endevu.

Aidha Naibu waziri ameitaka taasisi hiyo ya kidini baada ya kuandaa mpango kazi huo ugawiwe kwa uongozi wa idara ya mifugo Hamashauri ya Wilaya ya Sumbawanga,uongozi wa mifugo mkoa wa Rukwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi makao makuu kwa ajili ya kumbukumbu.

Mhe.Ulega ameseama¬† kuwa mpango huo utasaidia kufuatilia utekelezaji wake kuona kama wanafanya kazi kama mpango huo unavyoelekeza au la na kuweza kuchukua hatua stahiki kwa uongozi wa shamba ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa shamba hilo na kugawiwa kwa wafugaji endapo itagundulika hawafuati mpango kazi wa shamba hilo.

Akizungumzia mafanikio ya shamba hilo Naibu waziri alisema kuwa siya kuridhisha kwa kuwa tangu libinafsishwe nakupewa taasisi hiyo inaonekana kuna shughuli zingine nje ya zile za kuedekeza shamba hilo zinafanyika hivyo kutokuwa na mafanikio chanya.

“Haiwezekani hadi leo,2019 taasisi inaidadi ya ng’ombe 337 toka idadi ya ng’ombe 174 iliwakuta wakati wanapewa shamba hilo ,mwaka 2007”,alisema Ulega.

Awali akisoma taarifa ya shamba hilo Meneja Mchunguji Bw.Rwiza Binamungu alisema kuwa shamba hilo lina ukubwa wa hekta elfu kumi(10,000), ng’ombe wa maziwa 144 nauzalishaji wa maziwa kwa siku ni lita 50.

Hivi karibuni Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alishasema kuwa Mashamba ya serikali ambayo yanasuasua katika uzalishaji yagawiwe kwa wafugaji ili wafuge kibashara na kisasa.