Afisa Mfawidhi kutoka Brela kanda ya kusini ambaye ni mtaalamu wa mfumo wa usajili Francis Mwakalebela aliyesimama akitoa maelekezo kwa kwa njia ya vitendo washiriki wa mafunzo hayo kuhusina na namna ya kuweza kusajili makampuni ya na majina ya biashara kwa njia ya mtandao.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika zoezi la kujifunza jinsi ya kufanya usajili kwa kutumia mfumo wa mtandao
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani wakiwa wanaelekezana jinsi ya kuweza namna na kujisajili makampuni na majina ya biashra kwa kwa kutumia njia ya mtandao.
Wafanyabishara wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika mafunzo ya kujifunza namna ya kusajili makampuni na majina ya biashara kwa njia ya mtandao.
Afisa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya mji Kibaha Lea Lwanji kushoto akiwa na mshiriki mwenzake wakiwa wanafuatilia kwa umakini mafunzo ya usajili kwa kutumia mfumo wa njia ya mtandao
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa wanaangalia jinsi ya mfumo wa kujisajili kwa njia ya mtandao unavyofanya kazi
Moja ya bango la Brela ambalo linaonyesha maelezo kuhusiana na mfumo wa kufanya usajili kwa kutumia mfumo wa mtandao.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
……………………
VICTOR MASANGU, PWANI
BAADHI ya wafanyabiashara Mkoani Pwani ambao kwa kipindi cha muda mrefu waliokuwa wanakabiliwa na changamoto sugu ya kufanyiwa vitendo vya utapeli pindi wanapotaka kupatiwa usajili wa makampuni yao pamoja na majina ya biashara hatimaye wamepata ufumbuzi baada ya kupatiwa mafunzo maalumu kutoka Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) kwa lengo la kujifunza sheria na taratibu za usajili.
Wakizungumza katika ufunguzi rasmi wa mafunzo maalumu yaliyoandaliwa kwa umma juu ya kujifunza jinsi ya kutumia mfumo wa usajili wa makampuni na majina ya biashara baadhi ya wafanyabiashara hao akiwemo Abdala Ndauka na Elina Mgonja wamesema kwa miaka mingi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya upateli hivyo kujikuta wanaingia hasara kubwa katika zoezi zima la upatikanaji wa leseni.
Aidha wafanyabiashara hao wametoa pongezi kwa Brela kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa changamoto mbali mbali ambao ilikuwa zikiwakabili katika siku za nyuma katika kutekeleza majukumu yao hususan kuweza kutumia mfumo wa usajili wa kampuni na majina ya biashara zao.
“Kwa kweli sisi kama wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani tunatoa pongezi zetu za dhati kwa mamlaka husika ya Brela kwa kuona umuhimu ya kutupatia mafunzo hayo ya kujisajili kwa kutumia njia ya mtandao, maana hapo awali tulikuwa tunapata usiumbufu mkubwa na wakati mwingine kutapeliwa na baadhi ya watu hivyo kwa sasa tunaweza kutimiza majukumu yetu kwa weledi wa hali ya juu,”walisema wafanyabiashara hao.
Kwa upande wake mkurugenzi wa utawala na fedha kutoka Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA)Bakari Mketo alibainisha kwamba lengo la kuandaa mafunzo hayo kwa wafanyabiashara pamoja na umma kuhusina na kupata huduma za usajili kwa njia ya mtandao ikiwemo kuwajengea uwezo katika suala zima la ulipaji wa madeni kwa wateja wao ili kuondokana na usumbufu waliokuwa waliokuwa wanaupata.
“Lengo letu kubwa kwa sasa tunazunguka katika mikoa mbali mbali na kwa sasa tumeamua kuwakutanisha wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani ili tuweze kuwapa mafunzo maalumu ambayo yatawawezesha kuweza kujisajili kwa kutumia njia ya mtandao pamoja na kujifunza mambo mbali mbali ambayo yanahusiama ma utoaji wa leseni za viwanda,”alisema Mketo.
Pia alibainisha kwamba lengo lao kubwa ni kuweka mikakati kabambe ambayo iytaweza kuwasaidia wafanyabiashara kuondokana na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikiwakabili katika utekelezaji wa majukumu yao,ili waweze kufanya usajili wa makampuni yao pamoja na majina ya biashara zao bila ya kuwepo na usumbufu wowote.
Naye Afisa biashara mkuu kutoka Wizara ya viwanda na bishara Jane Lyatuu aliwataka wafanyabishara wote nchini kuhakikisha wanazisajili biashara zao zote pamoja na makampuni,taasisi, viwanda kwa lengo la kuweza kuhimili ushindani uliopo katika soka la bara la afrika kwa kuzingatia ubora wa bidhaa zinazotengezwa nchini.
KATIKA mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku mbili yalitolewa kwa umma juu ya kutumia mfumo wa usajili wa kampuni na majina ya biashra , pamoja na alma za bishara na utoaji wa leseni za viwanda yamewashirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo, maafisa biashara, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, maafisa maendeleo, mkaguzi wa ndani pamoja na wanasheria.
Afisa Mfawidhi kutoka Brela kanda ya kusini ambaye ni mtaalamu wa mfumo wa usajili Francis Mwakalebela aliyesimama akitoa maelekezo kwa kwa njia ya vitendo washiriki wa mafunzo hayo kuhusina na namna ya kuweza kusajili makampuni ya na majina ya biashara kwa njia ya mtandao.Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika zoezi la kujifunza jinsi ya kufanya usajili kwa kutumia mfumo wa mtandaoWashiriki wa mafunzo hayo kutoka maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani wakiwa wanaelekezana jinsi ya kuweza namna na kujisajili makampuni na majina ya biashra kwa kwa kutumia njia ya mtandao.Wafanyabishara wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika mafunzo ya kujifunza namna ya kusajili makampuni na majina ya biashara kwa njia ya mtandao.Afisa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya mji Kibaha Lea Lwanji kushoto akiwa na mshiriki mwenzake wakiwa wanafuatilia kwa umakini mafunzo ya usajili kwa kutumia mfumo wa njia ya mtandaoWashiriki wa mafunzo hayo wakiwa wanaangalia jinsi ya mfumo wa kujisajili kwa njia ya mtandao unavyofanya kaziMoja ya bango la Brela ambalo linaonyesha maelezo kuhusiana na mfumo wa kufanya usajili kwa kutumia mfumo wa mtandao.(PICHA NA VICTOR MASANGU)……………………VICTOR MASANGU, PWANI BAADHI ya wafanyabiashara Mkoani Pwani ambao kwa kipindi cha muda mrefu waliokuwa wanakabiliwa na changamoto sugu ya kufanyiwa vitendo vya utapeli pindi wanapotaka kupatiwa usajili wa makampuni yao pamoja na majina ya biashara hatimaye wamepata ufumbuzi baada ya kupatiwa mafunzo maalumu kutoka Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA) kwa lengo la kujifunza sheria na taratibu za usajili.Wakizungumza katika ufunguzi rasmi wa mafunzo maalumu yaliyoandaliwa kwa umma juu ya kujifunza jinsi ya kutumia mfumo wa usajili wa makampuni na majina ya biashara baadhi ya wafanyabiashara hao akiwemo Abdala Ndauka na Elina Mgonja wamesema kwa miaka mingi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya upateli hivyo kujikuta wanaingia hasara kubwa katika zoezi zima la upatikanaji wa leseni.Aidha wafanyabiashara hao wametoa pongezi kwa Brela kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa changamoto mbali mbali ambao ilikuwa zikiwakabili katika siku za nyuma katika kutekeleza majukumu yao hususan kuweza kutumia mfumo wa usajili wa kampuni na majina ya biashara zao.“Kwa kweli sisi kama wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani tunatoa pongezi zetu za dhati kwa mamlaka husika ya Brela kwa kuona umuhimu ya kutupatia mafunzo hayo ya kujisajili kwa kutumia njia ya mtandao, maana hapo awali tulikuwa tunapata usiumbufu mkubwa na wakati mwingine kutapeliwa na baadhi ya watu hivyo kwa sasa tunaweza kutimiza majukumu yetu kwa weledi wa hali ya juu,”walisema wafanyabiashara hao.Kwa upande wake mkurugenzi wa utawala na fedha kutoka Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA)Bakari Mketo alibainisha kwamba lengo la kuandaa mafunzo hayo kwa wafanyabiashara pamoja na umma kuhusina na kupata huduma za usajili kwa njia ya mtandao ikiwemo kuwajengea uwezo katika suala zima la ulipaji wa madeni kwa wateja wao ili kuondokana na usumbufu waliokuwa waliokuwa wanaupata.“Lengo letu kubwa kwa sasa tunazunguka katika mikoa mbali mbali na kwa sasa tumeamua kuwakutanisha wafanyabiashara wa Mkoa wa Pwani ili tuweze kuwapa mafunzo maalumu ambayo yatawawezesha kuweza kujisajili kwa kutumia njia ya mtandao pamoja na kujifunza mambo mbali mbali ambayo yanahusiama ma utoaji wa leseni za viwanda,”alisema Mketo.Pia alibainisha kwamba lengo lao kubwa ni kuweka mikakati kabambe ambayo iytaweza kuwasaidia wafanyabiashara kuondokana na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikiwakabili katika utekelezaji wa majukumu yao,ili waweze kufanya usajili wa makampuni yao pamoja na majina ya biashara zao bila ya kuwepo na usumbufu wowote.Naye Afisa biashara mkuu kutoka Wizara ya viwanda na bishara Jane Lyatuu aliwataka wafanyabishara wote nchini kuhakikisha wanazisajili biashara zao zote pamoja na makampuni,taasisi, viwanda kwa lengo la kuweza kuhimili ushindani uliopo katika soka la bara la afrika kwa kuzingatia ubora wa bidhaa zinazotengezwa nchini. KATIKA mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku mbili yalitolewa kwa umma juu ya kutumia mfumo wa usajili wa kampuni na majina ya biashra , pamoja na alma za bishara na utoaji wa leseni za viwanda yamewashirikisha wadau mbali mbali wa maendeleo, maafisa biashara, wafanyabiashara wadogo na wakubwa, maafisa maendeleo, mkaguzi wa ndani pamoja na wanasheria.