Home Mchanganyiko Wananchi wajitokeza kwa wingi katika Banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete...

Wananchi wajitokeza kwa wingi katika Banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kupima afya zao na kupata ushauri

0

Afisa Uuguzi wa chumba cha upasuaji kutoka  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edina Mulenda akieleza jinsi upasuaji wa moyo unavyofanyika kwa wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa bila malipo ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo.

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mkuu wa kitengo cha Utafiti na Mfunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa za shinikizo la juu la damu kwa  Mbaraka Samatta wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa bila malipo ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aisha Omary akimpima  kiwango cha sukari mwilini Joseph Karumuna wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa bila malipo huduma za ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo kwa wananchi wanaotembelea banda hilo lililopo katika banda la Jakaya Kikwete.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Consolata Minja akimpima shinikizo la damu (BP) Erick Nestory  wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo bila malipo kwaa watoto na watu wazima wanaotembelea banda hilo lililopo katika banda la Jakaya Kikwete.

Daktari wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Happiness Swai akitoa ushauri wa jinsi ya kuepukana na magonjwa ya moyo kwa  Anna Mtui wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa huduma za ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo bila malipo kwa wananchi  wanaotembelea banda hilo lililopo ndani ya  banda la Jakaya Kikwete.