Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akimpokea Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa alipowasili Mkoani humo kwa ziara ya siku moja
Waziri Bashungwa akiweka bayana kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Lengo la ziara yake alipomtembelea ofisini kwake.
Waziri wa Viwanda Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na mwenyeji wake Dkt. Kebwe Stephen Kebwe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakipokelewa na wenyeji wao katika kiwanda cha nguo cha 21C. cha Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya siku moja Juni 29 mwaka huu.
Kiwanda cha kutengeneza nguo cha 21st Centuary cha Mkoani Morogoro kinavyoonekana kwa ndani
………………………….
Na. Andrew Chimesela – Morogoro
Waziri wa Viwanda na Biashara hapa nchini Innocent Bashungwa amezitaka taasisi za SIDO, TIRDO, CAMATEC na TEMDO’S kuamka kutoka usingizini na kujikita katika kuandaa vijana na akinamama kupata ujuzi mbalimbali ili waweze kuajiriwa viwandani ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto kubwa iliyojitokeza wakati anatembelea viwanda Mkoani Morogoro.
Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo wakati wa ziar yake ya siku moja Mkoani Morogoro ikiwa na lengo la kutembelea viwanda vya kuchakata mazao ya wakulima ikiwemo kiwanda cha nguo cha 21st Centuary, kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo cha Mazava, na kiwanda cha Tumbaku cha TTPL ambavyo vyote viko katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Waziri Bashungwa amesema taasisi hizo za SIDO TIRDO, CAMATEC na TEMDO’S ambazo ziko chini ya Wizara yake ziliazishwa mahususi kwa ajili ya kutatua changamoto kama hizo zinazojitokeza viwandani na kuzitaka taasisi hizo kujikita katika kutoa ujuzi kwa Vijana na akinamama hasa ujuzi unaohitajika na viwanda hivyo ili waweze kuajiriwa huku akizitaka mamlaka hizo kwenda katika viwanda alivyotembelea ili kukaa pamoja na kutengeneza program zitakazofanikisha kuondoa changamoto hiyo.
“Mtaani wanatafuta ajira huku viwandani wanasema tunataka vijana wenye ujuzi wa namna hii na mimi ni Waziri wa Viwanda na Biashara, kwa hiyo nimeagiza SIDO, TIRDO, CAMATEC, na TEMDO’S ambao wako chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara waamke kutoka usingizini” amesema Waziri Bashungwa.
Agizo hilo limekuja baada ya Waziri Bashungwa kupokea changamoto ya aina moja kwa viwanda viwili kati ya vile alivyovitembelea kikiwemo kiwanda cha kutengeneza nguo cha 21st Centuary na kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo cha Mazava vya Mkoani Morogoro huku wamiliki wa viwanda hivyo wakilalamika kutumia muda mrefu kuwafundisha vijana hadi kufanikiwa kufanya kazi kwa ufanisi kiwandani.
na kusababisha Waziri kuagiza mamlaka hizo kufika katika viwanda alivyotembelea ili waweze kukaa pamoja na kutengeneza program zitakazofanikisha kuondoa changamoto hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Bashungwa amesema ni azma yake kutaka atatembelea viwanda vyote vya hapa nchini vinavyochakata mazao ya wakulima (Textile Industries) ili kujua changamoto zake na kuzitatua ili viwanda hivyo viweze kutimiza azma ya Serikali ya wakulima wa mazao ya pamba na tumbaku kupata bei nzuri na masoko ya uhakika.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ambaye aliambatana na Waziri huyo wakati wa ziara hiyo alizungumzia zaidi ufanisi na changamoto za Kiwanda cha tumbaku cha TTPL ambapo pamoja na kukiri kuwa Kiwanda kinafanya vizuri lakini ameiomba Serikari kuendelea na mazungumzo ili kutatua changamoto iliyopo kiwandani hapo ambayo tayari imeripotiwa ngazi ya Wizara.
Kwa upande wao wamiliki wa viwanda vya 21st Centuary na kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo cha Mazava kupitia risala iliyosomwa na meneja msaidzi wa Kiwanda cha Mazava Bw. Nelson Mchupya wamesema pamoja na mafanikio yaliyopo bado wanachangamoto, kubwa ni ukosefu wa wafanyakazi wenye ujuzi kwa kazi wanazotakiwa kuzifanya kiwandani hapo.
Huku Kiwanda cha Mazava kilichoazishwa mwaka 2018 na kujihusisha na kutengeneza nguo za michezo ambazo kinauzwa nchini Maerekani kwa asilimia mia kilianza na wafanyakazi 300 huku kikisafirisha kontena 40 za futi 40 sawa na wastani wa nguo laki moja kwa mwezi, kwa sasa kiwanda kimeajiri wafanyakazi 2,161 na kinasafirisha makontena 16 ya futi 40 sawa na nguo milioni moja kwa mwezi zinasafirishwa nchini Marekani.
Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akimpokea Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa alipowasili Mkoani humo kwa ziara ya siku mojaWaziri Bashungwa akiweka bayana kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Lengo la ziara yake alipomtembelea ofisini kwake.Waziri wa Viwanda Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na mwenyeji wake Dkt. Kebwe Stephen Kebwe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakipokelewa na wenyeji wao katika kiwanda cha nguo cha 21C. cha Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya siku moja Juni 29 mwaka huu.Kiwanda cha kutengeneza nguo cha 21st Centuary cha Mkoani Morogoro kinavyoonekana kwa ndani………………………….Na. Andrew Chimesela – MorogoroWaziri wa Viwanda na Biashara hapa nchini Innocent Bashungwa amezitaka taasisi za SIDO, TIRDO, CAMATEC na TEMDO’S kuamka kutoka usingizini na kujikita katika kuandaa vijana na akinamama kupata ujuzi mbalimbali ili waweze kuajiriwa viwandani ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto kubwa iliyojitokeza wakati anatembelea viwanda Mkoani Morogoro.Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo wakati wa ziar yake ya siku moja Mkoani Morogoro ikiwa na lengo la kutembelea viwanda vya kuchakata mazao ya wakulima ikiwemo kiwanda cha nguo cha 21st Centuary, kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo cha Mazava, na kiwanda cha Tumbaku cha TTPL ambavyo vyote viko katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.Waziri Bashungwa amesema taasisi hizo za SIDO TIRDO, CAMATEC na TEMDO’S ambazo ziko chini ya Wizara yake ziliazishwa mahususi kwa ajili ya kutatua changamoto kama hizo zinazojitokeza viwandani na kuzitaka taasisi hizo kujikita katika kutoa ujuzi kwa Vijana na akinamama hasa ujuzi unaohitajika na viwanda hivyo ili waweze kuajiriwa huku akizitaka mamlaka hizo kwenda katika viwanda alivyotembelea ili kukaa pamoja na kutengeneza program zitakazofanikisha kuondoa changamoto hiyo.“Mtaani wanatafuta ajira huku viwandani wanasema tunataka vijana wenye ujuzi wa namna hii na mimi ni Waziri wa Viwanda na Biashara, kwa hiyo nimeagiza SIDO, TIRDO, CAMATEC, na TEMDO’S ambao wako chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara waamke kutoka usingizini” amesema Waziri Bashungwa.Agizo hilo limekuja baada ya Waziri Bashungwa kupokea changamoto ya aina moja kwa viwanda viwili kati ya vile alivyovitembelea kikiwemo kiwanda cha kutengeneza nguo cha 21st Centuary na kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo cha Mazava vya Mkoani Morogoro huku wamiliki wa viwanda hivyo wakilalamika kutumia muda mrefu kuwafundisha vijana hadi kufanikiwa kufanya kazi kwa ufanisi kiwandani. na kusababisha Waziri kuagiza mamlaka hizo kufika katika viwanda alivyotembelea ili waweze kukaa pamoja na kutengeneza program zitakazofanikisha kuondoa changamoto hiyo.Katika hatua nyingine Waziri Bashungwa amesema ni azma yake kutaka atatembelea viwanda vyote vya hapa nchini vinavyochakata mazao ya wakulima (Textile Industries) ili kujua changamoto zake na kuzitatua ili viwanda hivyo viweze kutimiza azma ya Serikali ya wakulima wa mazao ya pamba na tumbaku kupata bei nzuri na masoko ya uhakika.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ambaye aliambatana na Waziri huyo wakati wa ziara hiyo alizungumzia zaidi ufanisi na changamoto za Kiwanda cha tumbaku cha TTPL ambapo pamoja na kukiri kuwa Kiwanda kinafanya vizuri lakini ameiomba Serikari kuendelea na mazungumzo ili kutatua changamoto iliyopo kiwandani hapo ambayo tayari imeripotiwa ngazi ya Wizara.Kwa upande wao wamiliki wa viwanda vya 21st Centuary na kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo cha Mazava kupitia risala iliyosomwa na meneja msaidzi wa Kiwanda cha Mazava Bw. Nelson Mchupya wamesema pamoja na mafanikio yaliyopo bado wanachangamoto, kubwa ni ukosefu wa wafanyakazi wenye ujuzi kwa kazi wanazotakiwa kuzifanya kiwandani hapo.Huku Kiwanda cha Mazava kilichoazishwa mwaka 2018 na kujihusisha na kutengeneza nguo za michezo ambazo kinauzwa nchini Maerekani kwa asilimia mia kilianza na wafanyakazi 300 huku kikisafirisha kontena 40 za futi 40 sawa na wastani wa nguo laki moja kwa mwezi, kwa sasa kiwanda kimeajiri wafanyakazi 2,161 na kinasafirisha makontena 16 ya futi 40 sawa na nguo milioni moja kwa mwezi zinasafirishwa nchini Marekani.