Home Mchanganyiko TANAPA YADHAMIRIA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII KANDA YA KUSINI NA KUWA KINARA...

TANAPA YADHAMIRIA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII KANDA YA KUSINI NA KUWA KINARA NCHINI

0

*******************

NJOMBE  

Shirika la hifadhi ya taifa TANAPA kanda ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania imezitaja changamoto za miundombinu,elimu duni pamoja na uvamizi katika maeneo ya hifadhi zilizopo katika kanda hviyo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya sekta hiyo nyeti inayochangia pato kubwa la taifa .

Kutokana na changanmoto hizo ambazo zinatajwa kukwamisha jitihada za serikali katika kutunza na kutangaza rasirimali za nchini hususani hifadhi za taifa , TANAPA limelazimika kukutana na kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mkoa ili kuweka mkakati wa pamoja utakaosaidia kuinua sekta ya utalii katika mikoa ya kusini ambayo inavivutio vingi vya aina yake .

Christopher Timbuka ambaye ni kamishina mwandamizi wa TANAPA kanda ya kusini pamoja na Teodola Royce ambaye ni mkuu wa hifadhi ya taifa ya kitulo wanaeleza dhamira ya kukutanisha kamati za ulinzi katika kikato hicho na kueleza maazimio yaliowekwa ili kumaliza changamoto ya uvamizi na,elimu pamoja na miundombinu hususani changamoto ya wizi wa mmea aina ya chikanda ambao umekuwa ukivunwa kwa wingi kinyemela na kusafirishwa nje ya nchi kwa madai ya kwamba ni dawa.

Awali akitanabaisha utajiri wa vivutio  vilivyopo mkoani Njombe wakati wa kufungua kikao hicho cha TANAPA na kamati za ulinzi mkuu wa mkoa huo Christopher Olesendeka amesema Njombe ina jiwe lenye ramani ya africa ,Ziwa, mapango ya kihistoria, misitu yenye maajabu , hifadhi na mengine mengi na kwamba serikali itafanya kila jambo kuhakikisha hifadhi zinatinzwa ili ziweze kuleta tija kwa taifa na kutoa agizo kwa wakuu wa wilaya na watumishi wengine .

Na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wilaya ya Wanging’ombe Comrade Ally Kassinge yenye pori tengefu la mpanga kipengele pamoja na msitu wa maajabu wa Nyumba nitu anaeleza hatua wanazokwenda kuchukua ili kutunza hifadha na vivutio.

Katika kanda ya nyanda za juu kusini TANAPA ina hifadhi tatu kubwa ambazo ni Ruaha iliyopo mkoani Iringa , huku Njombe ikiwa na hifadhi ya Kitulo na hifhadhi ya Katavu iiyopo Katavi