Home Mchanganyiko VIONGOZI WASTAAFU WA MAGEREZA KUZINDUA VITABU VIWILI VINAVYOELEZEA HISTORIA YA JESHI LA...

VIONGOZI WASTAAFU WA MAGEREZA KUZINDUA VITABU VIWILI VINAVYOELEZEA HISTORIA YA JESHI LA MAGEREZA

0

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akionesha vitabu viwili
ambavyo vimeandikwa na Viongozi Waandamizi wastaafu wa Jeshi la Magereza,
akiwemo Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Simon Mwanguku na Naibu Kamishna Mstaafu, John Nyoka, Viongozi hao wamekabidhi vitabu hivyo leo juni 24, 2019, Makao Makuu ya Magereza. Vitabu hivyo vinaelezea historia ya Jeshi la Magereza pamoja na Programu za Urekebishaji vinatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Viongozi Waandamizi wastaafu wa Jeshi la Magereza, akiwemo Kamishna Mkuu
wa Magereza Mstaafu wa Magereza, Simon Mwanguku(kushoto), Kamishna Mkuu
Mstaafu, Jumanne Mangala(katikati) na Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, John Nyoka(kushoto) wakiwa Ofsini kwa Kamishna Jenerali wa Magereza katika
mazungumzo maalum ya maandalizi ya uzinduzi wa vitabu viwili vinavyoelezea
historia ya Magereza pamoja na Programu ya Urekebishaji.

Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akiwa na
manaibu Kamishna wa Magereza kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo maalum ya maandalizi ya uzinduzi wa vitabu viwili vilivyoandikwa na Viongozi Waandamizi
wastaafu wa Magereza, leo Juni 24, 2019.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akizungumza na Viongozi
Waandamizi wastaafu wa Jeshi la Magereza(kulia), leo Juni 24, 2019, Makao Makuu ya Magereza. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Uwesu Ngarama akiwa na manaibu Kamishna wa Magereza kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo ya maandalizi ya uzinduzi wa vitabu viwili vilivyoandikwa na wastaafu wa Magereza(Picha na Jeshi la Magereza).